Nenda kwa yaliyomo

Sophie Turner

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sophie Turner
Amezaliwa21 Februari 1996
UtaifaMwingereza
Majina mengineSophie Belinda Turner
Kazi yakemwigizaji
Miaka ya kazi2009-hadi sasa
MwenzaJoe Jonas (m. 2019–2023) «start: (2019)–end+1: (2024)»"Marriage: Joe Jonas to Sophie Turner" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Sophie_Turner)
Watoto2

Sophie Belinda Turner (amezaliwa Februari 12, 1996)[1] ni mwigizaji wa Uingereza. Aliigiza kama Sansa Stark katika tamthilia ya Game of Thrones (2011-2019), ambapo ilimfanya ateuliwe kugombania tuzo za Emmy Awards kugombania katika fani ya Mwigizaji Bora katika Tamthilia mnamo mwaka 2019.

Turner aliigiza katika filamu ya Uingereza ya mwaka wa 2013 iliyoitwa The Thirteenth Tale na kumfanya kuwa filamu yake ya kwanza kuigiza, pia aliigiza katika tamthilia ya kisaikolojia iliyoitwa Another Me (2013). Aliigiza pia kwenye filamu ya ucheshi Barely Lethal (2015) na aliigiza kama kijana Jean Grey / Phoenix katika filamu ya X-Men (2016-2019).

Maisha Ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Sophie Belinda Turner alizaliwa Northampton[2] huko Uingereza tarehe 21 Februari 1996,akiwa ni binti yake Sally, mwalimu wa shule ya kulea watoto, na Baba yake Andrew, ambaye anafanya kazi katika kampuni ya usambazaji wa magodoro[3]. Alihamia Chesterton, Warwickshire alipokuwa na umri wa miaka 2. Alisoma katika Shule ya msingi ya Warwick hadi alipokuwa na umri wa miaka 11,na baadaye alihudhuria Shule ya Wasichana ya The King's inayojitegemea. Turner amekuwa ni mwanachama wa Kampuni ya Playbox Theatre tangu akiwa na umri wa miaka 3. Ana kaka wawili wakubwa[4][5]. Pacha wake alifariki akiwa bado tumboni mwa mama yake[6][7] [8].

Alilelewa katika nyumba kubwa ya Edwardian, karibu na Leamington Spa, akisema, "Utoto wangu ulikuwa wa kufurahisha sana. Tulikuwa na nguruwe, mazizi ya ng'ombe na farasi, na tulikuwa tukitambaa kwenye matope." Turner alikuwa na mwalimu wa filamu ya Game of Thrones hadi akiwa na umri wa miaka 16. Alipata daraja tano za GCSE A na nne za B, ikiwa pamoja na B katika Drama.

Maisha Binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Turner alianza kuwa na mahusiano na mwimbaji wa Marekani Joe Jonas mwaka 2016[9]. Walichumbiana mnamo Oktoba 2017[10] na kufunga ndoa tarehe 1 Mei 2019 huko Las Vegas, Nevada.[11] Wanandoa hao waliishi New York City kufikia Mei 2019[12]. Walifanya sherehe ya pili ya harusi huko Carpentras, Ufaransa tarehe 29 Juni 2019. Wanandoa hao wana watoto wawili wakike, waliozaliwa Julai 2020 na Julai 2022[13][14]. Turner ndiye alimhamasiha mpenzi wake Jonas amtungie wimbo wa "Hesitate", ulioandikwa kama barua ya mapenzi kwake na Jonas, kwa ajili ya albamu ya Brothers reunion album, Happiness Begins.

Mwanzoni mwa mwezi Septemba 2023, Jonas aliwasilisha kesi ya talaka kutoka kwa Turner huko Miami, Florida. Hili taarifa ilithibitishwa na Turner na Jonas kupitia Instagram kuwa ni uamuzi wa pande zote. Baadaye mwezi huohuo Turner alimshtaki mume wake aliemtaliki (Jonas) iliaweze kuwaruhusu binti zao, waliozaliwa Marekani, warudi Uingereza, kwa vile waliwah kusajili makazi ya mume wake wa zamani kama makazi yao ya kudumu mnamo Aprili mapema mwaka huo. Jonas na Turner walifikia makubaliano ya malezi kwa muda mnamo Oktoba.

  1. "Interview with Sophie Turner - Winter Is Coming". web.archive.org. 2011-04-02. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-14. Iliwekwa mnamo 2024-04-30. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |dead-url= (help)
  2. Condé Nast (2016-06-01). "10 things you need to know about Sophie Turner". Vogue France (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  3. "An Interview with Sophie Turner of Game of Thrones for the Spring 2015 issue of Town & Country | Town & Country Magazine UK". web.archive.org. 2015-02-01. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-16. Iliwekwa mnamo 2024-04-30. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. Catherine Vonledebur (2013-08-16). "Look: Leamington Game of Thrones actress Sophie Turner enjoying her rise to fame". Coventry Live (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  5. "Playbox Theatre Alumni". Playbox Theatre (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  6. "Game of Thrones's Sophie Turner: 'I’ve grown up with Sansa Stark - I really feel what she feels'". The Telegraph (kwa Kiingereza). 2015-04-13. Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  7. "Game of Thrones's Sophie Turner: 'I’ve grown up with Sansa Stark - I really feel what she feels'". The Telegraph (kwa Kiingereza). 2015-04-13. Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  8. https://www.bbc.co.uk/mediacentre/mediapacks/thirteenthtale/sophie-turner.html
  9. Hannah Hargrave (2016-11-07). "Joe Jonas and Sophie Turner Kiss and Cuddle in the Netherlands". Us Weekly (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  10. http://www.nydailynews.com/entertainment/gossip/joe-jonas-sophie-turner-announce-engagement-instagram-article-1.3564728
  11. "Joe Jonas and Sophie Turner Get Married in Surprise Vegas Ceremony". Entertainment Tonight (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  12. Times, Josh Glancy | The Sunday (2024-05-01), Game of Thrones star Sophie Turner on how therapy helped her survive teen fame (kwa Kiingereza), ISSN 0140-0460, iliwekwa mnamo 2024-04-30
  13. Lucy Wood published (2019-07-01). "Every Detail From Sophie Turner and Joe Jonas' French Wedding". Marie Claire Magazine (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  14. https://www.bbc.co.uk/mediacentre/mediapacks/thirteenthtale/sophie-turner.html