Sophia Mbeyela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Sophia Mbeyela (amezaliwa tar.) ni mwanamke Mtanzania ambaye, pamoja ya kuwa na uwezo wa kuelimisha jamii, pia ameweza kujitoa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu walio katika makundi matatu nayo ni albino, walemavu wa viungo na yatima. [1][2]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Sophia alisoma katika shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu iliyopo jiji la Dar es Salaam ambapo alihitimu darasa la saba mwaka 2002. Baada ya kuhitimu, Sophia alipata nafasi ya kuendelea na shule ya sekondari. Aliweza kuendelea na shule mbalimbali ikiwemo shule ya Sekondari Jangwani. Badae pia aliweza kujiunga na chuo. [3]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Sophia ni mwalimu wa shule za sekondari nchini. [4] Ni mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali kwa watu wenye ulemavu(PLPDF).Amefanikiwa pia kua ni mwanzilishi wa asasi ya Madam Sophy Charity. Taasisi hii aliyoianzisha Sophia, ni taasisi isiyo ya kiserikali inayodhamiria kujishughulisha kutimiza malengo ya kusaidia watu walio na mahitaji maalumu ili kuweza kuwatia moyo ili waweze kujiona ni sawa kama watu wengine ili badae waweze kuwa mabalozi wazuri. [5]

Mafanikio[hariri | hariri chanzo]

Kwa kupitia taasisi yake ya Madam Sophy, Sophia ameweza kutembelea baadhi ya shule za sekondari ikiwemo shule ya sekondari ya Jangwani iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo alifanikwa kutoa kutoa msaada wa vitabu vya masomo mbalimbali. [6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sophia Mbeyela kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.