Sophia Kianni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kianni akizungumza kwenye mgomo wa hali ya hewa wa Ijumaa Nyeusi mnamo 2019

Sophia Kianni (amezaliwa 13 Disemba 2001) ni mwanaharakati wa hali ya hewa wa Marekani aliyebobea katika vyombo vya habari na mikakati. Yeye ndiye mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa asasi ya Climate Cardinals yenye kushughulika na utetezi wa mazingira. Climate Cardinals ni shirika lisilo la faida linaloongozwa na vijana ambalo hufanya kazi kutafsiri habari juu ya mabadiliko ya hali ya hewa katika lugha zaidi ya 100. Anaiwakilisha Marekani kama mwanachama mchanga zaidi kwenye Kikundi cha Ushauri cha Vijana cha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Tabia ya nchi.

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sophia Kianni kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.