Sogea Karibu
"Sogea Karibu" | ||
---|---|---|
Wimbo wa Juwata Jazz Band
kutoka katika albamu ya Mpenzi Zarina | ||
Umetolewa | 1979 | |
Umerekodiwa | 1979 | |
Aina ya wimbo | Muziki wa dansi | |
Lugha | Kiswahili | |
Urefu | 8:48 | |
Studio | RTD | |
Mtunzi | Kakere Belesa | |
Mtayarishaji | Juwata Jazz Band | |
Mpenzi Zarina orodha ya nyimbo | ||
|
Sogea Karibu ni jina la wimbo wa muziki wa dansi uliotungwa na Kakere Belesa na kuimbwa na Hassan Bitchuka kwa ajili ya Juwata Jazz Band mnamo 1979. Wimbo huu unasifika sana kwa kinanda (organ) chake cha huzuni kilichopigwa na mpigaji nguli wa "The Kilimanjaro Band", Waziri Ally (Kissinger). Sababu zilizopelekea kupiga organ katika wimbo huu, ni kuwa wapigaji wa vyombo vya upepo waligoma (tarumbeta na sax) kwa kuuona wimbo ni mbaya. Lakini baada ya kutoka wote walishangazwa na utamu uliopatikana katika wimbo huu. Sauti kuu ya wimbo huu imeimbwa na Hassan Rehani Bitchuka kwa ustadi wa hali ya juu. Ni moja kati ya nyimbo zilizotamba sana za Juwata Jazz Band kwa kipindi cha miaka ya 1970 na 1980 mwanzoni.
Wimbo unahusu mke mwema aliyekuja kubadilika tabia zisizovumilika katika ndoa. Mwishowe anamtaka abebe kilicho chake heri abaki mwenyewe. Wimbo umeimbwa kwa huzuni wa hali juu kabisa kwa muziki wa dansi wa kipindi hiko. Wimbo huuu ulikuwa utunzi wa Kakere Belesa, Kakere na Bitchuka walikuwa wanaishi nyumba moja ya kupanga miaka hiyo, Kakere alipompa Bitchuka wimbo huu, Bitchuka akafanya marekebisho madogo hasa yale maneno ya mwanzoni mwa wimbo sogea karibu Kakere alikuwa anaimba, Bitchuka akapendekeza heri iwe ya kuongea badala ya kuimba.
Baada ya hatua hiyo kwisha, wakaupeleka kwa wenzao ili wauanzie mazoezi, lakini watu wa ala za upepo chini ya uongozi wa Joseph Lusungu waliususia wimbo huu. Lakini baada ya kutoka wote waliukubali. Licha ya uwezo mkubwa wa Kakere wa kuimba, bado aliona wimbo huu ampatie sahib wake. Hii inadhihilisha ya kwamba wasanii wa zamani hawakuwa na choyo katika kufikisha ujumbe kwa hadhira husika. Uwezo wa Kakere unaweza kuusikia katika wimbo kama vile Asia, Chande, Baby Wangu - zote akiwa Bima.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Sogea Karibu katika YouTube