Nenda kwa yaliyomo

Soddo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muonekano wa Sodo.

Soddo au (Wolaita Sodo) ni mji uliopo kusini-kati mwa Ethiopia. Ilikuwa ni sehemu ya Sodo Wearda ya zamani ambayo ilihusisha Sodo Zuria.

Sodo ina kiwanja cha ndege na barabara yenye urefu wa kilomita 166 (maili 103) inayounganisha Sodo na Chida, ambayo ujenzi wake ulianza mnamo 1994, ilikamilishwa mapema 1999. Ikiwa na daraja la Bailey la mita 80 (futi 260) lipitalo juu ya mto Omo na madaraja mengine matano, inapunguza umbali kati ya mji mkuu wa mkoa huko Awassa na Mizan Teferi hadi kilometa 400 (mi 250).

Kufikia mwaka 2003 huduma za Sodo ni pamoja na upatikanaji wa simu, huduma ya posta, huduma ya umeme ya masaa 24, benki mbili, na hospitali. Sodo pia ni makao makuu ya Jimbo Katoliki la Soddo-Hosana. Hivi sasa, Sodo inajulikana kwa kuwa kituo cha taasisi kuu za afya na elimu nchini Ethiopia. Hospitali ya Kikristo ya Soddo ina moja ya vituo 10 vya mafunzo ya upasuaji katika Afrika. Hospitali hutoa huduma kamili za matibabu, na upasuaji, pamoja na Mifupa na Ujumla na Uzazi. Hospitali ya Rufaa ya Chuo Kikuu cha Wolaita Sodo pia iko katika mji huu na inahudumia watu karibu milioni mbili. Jumla ya vitanda hospitalini hapo vipo 200; vitanda 60 vilikuwa katika idara ya uzazi na magonjwa ya wanawake.

Mwanzoni mwa miaka ya 1930, Sodo ilielezewa kama eneo pekee katika wilaya ya Wolaita linalostahili kuitwa mji. Ilikuwa na soko la Jumamosi na utoaji wa barua kila wiki,kufikia mwaka 1958 Sodo ilikuwa moja ya maeneo 27 nchini Ethiopia iliyoorodheshwa kama Miji ya Daraja la Kwanza. Tawi la Benki ya Biashara ya Ethiopia lilianzishwa kati ya mwaka 1965-1968. Msimamizi wa Sodo Zuria wearda na mwanaharakati wa wanafunzi, Melaku Gebre Egziahber, alikamatwa mnamo 1975 kwa kuhamasisha wakulima na maskini wa mijini kujitokeza dhidi ya "wanyonyaji" katika mji huo. Mnamo 1984, kambi ya wakimbizi ilianzishwa katika mji huo kwa wahanga wa njaa ya mwaka huo.

Mwaka 2016 idadi ya wakazi ilikadiriwa kuwa 253,322[1]).

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Ethiopia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Soddo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.