Awasa
Awasa (pia Awassa au Hawassa, Kige'ez አዋሳ) ni mji mkuu wa Jimbo la Mataifa ya Kusini katika kusini ya Ethiopia. Iko kando la Ziwa Awasa katika Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki takriban kilomita 280 kusini ya Addis Abeba.
Mwaka 2005 Awasa ilikuwa na wakazi 125,315.[1]
Kati ya wakazi wake 69,169 wa mwaka 1994 asilimia 31,42 % walikuwa Waamhara, 24,91 % Wawelaytta, 11,55 % Waoromo, 10,2 % Wasidama, 4,85 % Wakambaata, 4,6 % Watigray, 3,23 % Soddo-Gurage, 2,15 % Wasilt'e, 2,13 % Sebat-Bet-Gurage und 1,56 % Wahadiyya.
63,42 % walisema Kiamhara kama lugha ya kwanza. [2]
Kiasili eneo la Awasa ilikuwa na misitu minene na hadi leo kuna miti mikubwa upande wa kaskazini na magharibi wa mji. Kuna maji mengi kwa hiyo watu wengi kutoka nyanda za juu walihamia hapa.
Awasa ilikuwa mji mkuu wa jimbo la awali la Sidamo. [3]
Barabara kuu kati na Addis Abeba na Nairobi inapita Awasa.
Uvuvi katika ziwa ni sehemu muhimu ya uchumi kwa wenyeji.
Kuna vyuo viwili ambavyo ni Awasa Adventist College na Chuo Kikuu cha Awasa.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Central Statistical Agency: 2005 National Statistics, Section–B Population Ilihifadhiwa 13 Novemba 2009 kwenye Wayback Machine., Table B.4 (PDF)
- ↑ CSA: The 1994 Population and Housing Census of Ethiopia: Results for Southern Nations, Nationalities and Peoples’ Region, Volume I: Part I. Statistical Report on Population Size and Charateristics Ilihifadhiwa 15 Novemba 2010 kwenye Wayback Machine., 1996 (p. 154, 196)
- ↑ Mekete Belachew: Awasa, in: Siegbert Uhlig (ed.): Encyclopaedia Aethiopica, vol. 1, 2003, ISBN 978-3447047463
Makala hii kuhusu maeneo ya Ethiopia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Awasa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |