Nenda kwa yaliyomo

Grife

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Slate)
Grife ya buluu
Grife ya kibichi (6 cm X 4 cm)

Grife (ing. slate) ni mwamba metamofia. Imeundwa kutoka kwa mwambatope iliyoathiriwa na shinikizo kubwa na joto. Mwambatope wenyewe ni mwamba mashapo unaotokana na matope ya udongo wa mfinyanzi ukipasuka kirahisi kwa bapa nyembamba. Tabia hiyo ya kupasuliwa kirahisi inaendelea katika grife kwa kuwa chini ya shinikizo na joto la wastani.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Bapa za grife inatumiwa katika nchi nyingi sawa na vigae vya kuezeka paa au kufunika kuta za nyumba zinazokingwa hivyo dhidi ya mvua. Bapa nzito zaidi zinafaa kwa kufunika sakafu ya jengo au pia kwa kupata uso nyororo wa njia ya kutembea.

Sleti za grife zilitumiwa katika nchi nyingi kama bao za mkononi au ukutani kwa kuandika shuleni.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Grife kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.