Nenda kwa yaliyomo

Simone de Beauvoir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Simone de Beauvoir
Simone de Beauvoir pamoja na Sartre na Che Guevara
Simone de Beauvoir pamoja na Sartre na Che Guevara
Alizaliwa 9 Januari 1908 (Paris)
Alikufa 14 Aprili 1986 (Paris)

Simona de Beauvoir alikuwa mwandishi na mwanafalsafa wa kike nchini Ufaransa. Alijulikana kwa sababu aliandika juu ya hali ya wanawake katika jamii akachunguza jinsi walivyokandamizwa na juu ya njia ya kuondoka katika hali hii.

Kwa miaka mingi aliishi pamoja na mwanafalsafa Jean-Paul Sartre.

Aliona ya kwamba hali ya mwanamke si jambo la maumbile bali ya jamii na masharti yake. Aliandika "Mtu haziliwi kama mwanamke, anafanywa hivyo". Alipinga ya kwamba wanawake wanatazamiwa kama "jinsia ya pili" kwa sababu ni wanaume walioanzisha majadiliano na mafundisho juu ya jinsi na kuunda kanuni zake wakijitazama wenyewe kama hali ya kawaida na wanawake kama hali ya pekee isiyo kawaida.

Viungo va Nje

[hariri | hariri chanzo]