Jean-Paul Sartre
Mandhari
Jean-Paul Sartre (21 Juni 1905 – 15 Aprili 1980) alikuwa mwandishi na mwanafalsafa kutoka nchi ya Ufaransa. Alikuwa mtetezi mkuu wa falsafa ya "Existentialism". Falsafa hiyo inakiri kwamba hakuna mantiki ambayo mtu angeweza kuitumia kwa ajili ya maamuzi yake, lakini lazima kila mtu afanye uchaguzi yeye mwenyewe na atawajibika kwa matendo yake. Mwaka wa 1964 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi lakini aliikataa.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jean-Paul Sartre kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |