Nenda kwa yaliyomo

Siku Njema (riwaya)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Siku Njema(riwaya))

Siku Njema ni riwaya ya Kiswahili iliyotungwa na mtunzi kutoka nchini Kenya aitwae Ken Walibora. Riwaya hii ilichapishwa mwaka 1996.

Riwaya hii inahusu maisha ya kijana mdogo aitwae Msanifu kombo ambae alizaliwa Tanga nchini Tanzania. Kijana huyu anakumbana na matatizo ya kifamilia akiwa anaishi na mama pekee mwenye kipaji cha kuimba taarab. Kuzaliwa nje ya ndoa kwa kijana huyu kunamfanya apitie changamoto nyingi kutoka kwa marafiki zake wa shuleni kutokana na tamaduni zao kuwa yeye sio mtoto halali.