Siana Nkya
Siana Nkya ni mtafiti na mwanataaluma wa jenetikia ya binadamu, hasa kwenye ugonjwa wa selimundu.
Kwa sasa ni mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).[1][2]Nkya pia ni mwanzilishi wa chama cha wataalamu wa maswala jenetiki za binadamu Tanzania (THGO) ambapo ndio raisi wa kwanza wa chama hicho. [3][4]
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Nkya alipata shahada ya uzamili kutoka MUHAS mwaka 2016 ambapo alifanya utafiti kwa kushirikiana na King’s College, London. Utafiti wake ulijikita kutafiti sababu za kijenetiki kwenye hemoglobini za vijusi. Moja ya mafanikio ya masomo yake ya uzamili ni kuanzisha kanzidata ya watu 1700 wenye ugonjwa wa selimundu.[5][6]
Wakati wa masomo ya uzamili alifanya utafiti kwa kutumia taarifa za kijenetiki za waafrika kwa njia ijulikanayo kama Genome Wide Association (GWAS) kwa mara ya kwanza kwa ushirikiano na taasisi ya Wellcome Trust Sanger.[6]
Ana shahada ya uzamivu ya Baolojia ya Molekuli kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 2007. Kama sehemu ya mafunzo yake ya shahada ya uzamivu alifanya utafiti kuhusu malaria akilenga alama usugu za kimolekuli za huko P. falciparum kwa kushirikiana na kituo cha utafiti cha Kemri Wellcome Trust, Kilifi, Mombasa, Kenya. Wakati huo huo, alihusika na kuanzisha ptogramu ya kupima watoto selimundu kwa watoto wachanga. [6]
Pia alipata shahada ya kwanza kwenye Mikrobiolojia na Kemia kutoka UDSM mwaka 2004.[7]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Nkya ni mhadhiri mwandamizi wa MUHAS ambapo ameanza kazi rasmi mwaka 2022. Kabla ya hapo alifanya kazi chuo ya ualimu cha Dar es Salaam (DUCE), UDSM huku akiwa honorary lecturer MUHAS.[6]
Miradi ya kisayansi
[hariri | hariri chanzo]- SPARCO
- SCD Program
- Sickle Charta
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- Fogarty Global Health Fellowship (2016/2017)[6](2018-2020)
- American Society of Hematology Global Research Award (2018-2020)
- Emerging Global Leader award by Fogarty International Center (FIC) (2019-2024)
- International Centre for Genetic Engineering and Biotechnology (ICGEB) (2020-2023)
- Commonwealth Split-Site Fellowship[6]
- African Academy of Science affiliate(2018-2022)[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Dr. Siana Nkya (Research Technical Lead) | https://www.sickleinafrica.org". www.sadacc.org. Iliwekwa mnamo 2024-05-04.
{{cite web}}
: External link in
(help)|title=
- ↑ "Siana Nkya". scholar.google.com. Iliwekwa mnamo 2024-05-04.
- ↑ "About us – Tanzania Human Genetics Organization" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-05-04.
- ↑ "Dr. Siana Nkya (Research Technical Lead) | https://www.sickleinafrica.org". www.sadacc.org. Iliwekwa mnamo 2024-05-04.
{{cite web}}
: External link in
(help)|title=
- ↑ "Dr. Siana Nkya (Research Technical Lead) | https://www.sickleinafrica.org". www.sadacc.org. Iliwekwa mnamo 2024-05-04.
{{cite web}}
: External link in
(help)|title=
- ↑ 6.0 6.1 6.2 6.3 6.4 6.5 6.6 "Biography". H3Africa Website. Iliwekwa mnamo 15 Machi 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Siana Nkya – H3Africa" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-05-04.