Chuo Kikuu cha Muhimbili
Chuo Kikuu cha Muhimbili | |
---|---|
Kimeanzishwa | 1963 |
Aina | Chuo kikuu cha umma |
Mwenyekiti | Mariam Mwafisi |
Chansela | Ali Hassan Mwinyi |
Walimu | 306 |
Wanafunzi | 3,861 |
Mahali | Dar es Salaam, Tanzania |
Tovuti | muhas.ac.tz |
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (kwa Kiingereza: Muhimbili University of Health and Allied Sciences; kifupi: MUHAS) chuo kikuu cha umma kilichopo Dar es Salaam, Tanzania. Ni taasisi kubwa ya afya na elimu ya afya huko Dar es Salaam Tanzania.
Kilipewa hadhi ya kuwa chuo kikuu mwaka 2007[1] Kabla ya hapo, kama Chuo cha Elimu ya Afya kilikuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Neno Muhimbili limetokana na neno la Kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza Wazaramo walisema "Hapo ndipo wanawake wanapokwenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa hivyo, nalo ladumu hadi leo.
Kwa leo hii Muhimbili ina shule ya madaktari, wauguzi, mafamasia, waganga wa meno, maafisa afya mazingira, maafisa mazingira na elimu ya juu ya afya.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Chuo kikuu cha Muhimbili kilianzishwa mwaka 1963, kilifunguliwa kama chuo cha afya Dar es Salaam ndani ya hospitali iliyoitwa Princess Margaret Hospital na wanafunzi 10 waliofuata kozi za uganga au upasuaji.
Mwaka 1968 kikafanywa ni kitengo cha tiba katika Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Tangu 2007 imeandikishwa kama Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili.
Ndani ya chuo kuna idara nne na taasisi tano.
Idara nne ni kama zifuatazo:
- Idara ya utaalamu wa meno
- Idara ya uganga
- Idara ya uuguzi
- Idara ya madawa
Kati ya taasisi kuna taasisi za afya ya umma na uganga wa kimila.
Mahali
[hariri | hariri chanzo]Mpaka mwaka 2018, chuo kina matawi mawili:
- Tawi kuu, lililopo barabara ya Umoja wa Mataifa mtaa wa Upanga Magharibi, katika jiji la Dar es Salaam.[2]
- Tawi la Mloganzila, lililopo umbali wa kilomita 31 kutoka tawi kuu.
- Chuo kina eneo la mafunzo katika mji wa Bagamoyo
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Chuo Kikuu cha Muhimbili | Chuo Kikuu cha Muhimbili". www.muhas.ac.tz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-06. Iliwekwa mnamo 2019-11-06.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help) - ↑ Chuo Kikuu cha Muhimbili (2017). "Historia ya chuo kikuu cha Muhimbili". Dar es Salaam. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-11. Iliwekwa mnamo 1 Juni 2018.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); Unknown parameter|=
ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Kigezo:Vyuo vikuu vya Tanzania
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Muhimbili kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |