Shule ya Kimarekani ya Marrakesh
Shule ya Kimarekani ya Marrakesh (ASM) ni shule isiyo ya kibiashara, inayojitegemea huko Marrakech, nchini Moroko. Ina madarasa kuanzia chekechea hadi daraja la 12.
Historia yake
[hariri | hariri chanzo]Shule ya Kimarekani ya Marrakesh ilianzishwa mnamo mwaka 1995 na Joseph A. McPhillips III, Mkuu wa Shule katika Shule ya American School of Tangier kwa miaka thelathini na tano. Ilianzishwa kama tawi la Shule ya The American School of Tangier, ambayo ilikuwepo tangu mwaka 1950, Shule ya kimarekani ya Marrakesh ilikusudiwa na Bwana McPhillips kuwa taasisi ya mfano, ikionyesha imani yake binafsi katika elimu na imani katika Ufalme wa Moroko .[1]
Mapema katika uongozi wa Joe McPhillips naBi Audrey Riffi, shule hiyo ilifungua milango yake katika vituo vya kukodi katika villa wakiwa na walimu wawili. Ilihamia katika kituo chake cha sasa ambacho ndo kilikuw ndo chanzo na kama hatua ya kwanza. Shule ya Chini ilifunguliwa mnamo Septemba 15, mwaka 2001, na Shule ya Juu ilifunguliwa mnamo Machi 27, mwaka 2002. Waliongeza madarasa kila mwaka, ASM ilimaliza darasa lake la kwanza kama mwandamizi mnamo 2008[1]
Mtaala
[hariri | hariri chanzo]Taasisi huru na ya binafsi iliyoko nje kidogo ya Marrakech, Moroko, ASM inatoa lugha ya Kiingereza, elimu ilikyokuwa na mfumo na mitaala ya kimarekani kutoka chekechea hadi darasa la 12. Shule hiyo inafuata viwango vya AERO (American Education Reaches Out). ASM imeidhinishwa kikamilifu na Jumuiya ya Kati ya Vyuo Vikuu na Shule. Wanafunzi lazima wasome miaka minne ya hesabu, miaka minne ya Kiingereza, miaka minne ya Historia, na miaka minne ya Sayansi ili kuhitimu. Kiarabu hutolewa katika Daraja la K-12 wakati Kifaransa huletwa katika Daraja la 2. Lugha zote mbili huzingatiwa kama masomo ya msingi ya mtaala ambayo wanafunzi wote wanatakiwa kuchukua. Ili kuwapa wanafunzi wanaojiunga na shule hiyo bila Kifaransa au Kiarabu kidogo, Shule hutoa viwango kadhaa: Advanced, Standard na Kiarabu / Kifaransa kwa wale wanaoanza.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Official website
- Eduoasis, Eduoasis (2016-04-27). "US Embassy Website". US Embassy Morocco. US Embassy. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-23. Iliwekwa mnamo 2016-04-27.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shule ya Kimarekani ya Marrakesh kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |