Shane
Shane | |
---|---|
Imeongozwa na | George Stevens |
Imetayarishwa na | George Stevens |
Nyota | Alan Ladd Jean Arthur Van Heflin Brandon deWilde Jack Palance |
Muziki na | Victor Young |
Imehaririwa na | William Hornbeck Tom McAdoo |
Imesambazwa na | Paramount Pictures |
Imetolewa tar. | Aprili 23, 1953 |
Ina muda wa dk. | Dakika 118 |
Nchi | Marekani |
Lugha | Kiingereza |
Bajeti ya filamu | Dola milioni 3.1 |
Mapato yote ya filamu | $20,000,000[1] |
Shane ni filamu ya mwaka wa 1953 kutoka nchini Marekani. Ipo katika mtindo wa filamu za western yenye muundo wa Technicolor kutoka kwa wasambazaji Paramount,[2][3] inafahamika sana kwa mandhari yake yaliyochezewa filamu, uhariri, uchezwaji, na mchango wake katika mtindo huu.[4] Filamu ilitayarishwa na kuongozwa na George Stevens huku muswaada andishi ikiandikwa na A. B. Guthrie, Jr.,[5] iliyotokana na riwaya ya mwaka wa 1949 yenye jina sawa ya Jack Schaefer.[6] Ushindi wake wa sinematografia umeenda kwa Loyal Griggs. Nyota wa filamu ya Shane ni Alan Ladd, Jean Arthur (katika ushiriki wake wa mwisho, na ya rangi pekee, katika kazi yake ya filamu) na Van Heflin, na uwepo wa Brandon deWilde, Jack Palance, Emile Meyer, Elisha Cook, Jr., na Ben Johnson.
Shane iliwekwa Na. 45 katika toleo la mwaka wa 2007 la orodha ya AFI's 100 Years...100 Movies, na Na. 3 kwenye AFI's 10 Top 10 katika kundi la 'Western'.
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Shane (Alan Ladd), ni mpiganaji mwenye weledi wa kutumia silaha na asiyependa kuongea sana ambaye maisha yake ya wali yamezingwa na siri nzito,[4] anaelekea katika kijiji kilichopo pembezoni mwa mji katika mabonde ya mji wa Wyoming, muda fulani baada ya Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani. Wakati wa chakula cha usiku na mkulima mwenyeji wa mji huo Joe Starrett (Van Heflin) na mkewe Marian (Jean Arthur), anagundua ya kwamba vita ya vitisho inaendelea katika wakazi wa mabondeni hapo. Ingawa wanamiliki ardhi hiyo kihalali chini ya kifungu cha umiliki wa ardhi cha Homestead Acts, mmiliki katili wa ng'ombe, Rufus Ryker (Emile Meyer), amekodisha wahuni na wasaidizi wengine ili kuwasumbua wakazi wa mabondeni hapo waondoke katika eneo hilo. Starrett anampa kazi Shane, anaikubali.
Katika duka kuu la kijiji, Shane na wanakijiji wengine wanapakia vifaa vya matumizi ya nyumbani. Shane anaingia katika baa pembezoni mwa duka, ambako watu wa Ryker wanakunywa, na kuagiza soda kwa ajili ya mtoto wa Starretts, Joey (Brandon deWilde). Chris Calloway (Ben Johnson), mmoja kati ya watu wa Ryker, anamwagia whiskey kwenye shati lake Shane. "Nukia kama mwanamume!" anamtania. Shane hajaingia mtegoni humo, akaachana na utani wa watu wa Ryker. Safari iliyofuata ya kuja mjini, Shane anarudi na chupa tupu kwa ajili ya soda baa pale, ambako Calloway anamfanyia tena istizahi. Shane anaagiza vikombe viwili vya whiskey, moja anammiminia Calloway katika shati na nyingine usoni, kisha kumpa kichapo hadi chini. Wengine wakalianzisha; Shane kakomaa nao, kwa msaada wa Starrett wakawashinda. Ryker anatangaza mikwara "safari ijayo mzozo utaambatana na moshi wa risasi."
Joey kapendezewa na Shane, na bunduki yake. Shane anamwonesha namna ya kuvaa kikoba cha kutunzi bastola na mafunzo ya kupiga risasi kwa haraka, lakini Marian anaingilia kati mafunzo hayo. Bunduki, anasema, hazitokuja kuwa sehemu ya maisha ya mtoto wake. Shane anajibu bunduki ni chombo, hakina ubora wala ubaya kuliko jembe au shoka, na kinaweza kuwa kibaya au kizuri inategemea na mtu anayekitumia. Marian anajibu ya kwamba mashamba hayo yatakuwa salama bila hata bunduki ikiwa na pamoja na Shane.
Jack Wilson (Jack Palance), mpiganaji wa kutumia bunduki mwenye uzoefu wa hali ya juu anakodiwa na Ryker, kwa makusudi anamchokoza Frank "Stonewall" Torrey (Elisha Cook, Jr.), kwa maneno ya kifedhuri na hatimaye kupandisha mori na pale mkulima huyu asiye-na-uzoefu alipojaribu kuifikia bunduki yake ili amuue Jack, hakufua dafu na hatimaye Wilson kamuulia mbali mkulima huyo. Mazikoni kwa Torrey, kuna mazungumzo miongoni mwa wakazi hao kundoka katika eneo hilo na kumwachia tu Ryker na wao wende zao; lakini baada ya kitendo cha watu wa Ryker kuwasha moto nyumba ya marehemu, punde wakapata mwongozo mpya nao si mwingine bali kupigania haki yao na kuendeleza mapambano.
Ryker anamwalika Starrett mkutanoni kujadili suala la makazi katika baa—kisha kumuagiza Wilson amuue pindi tu afikapo. Calloway, amechoshwa na mwenendo wa Ryker, anamwonya Shane huko kuna kudhulumiana. Starrett anakomaa kivyovyote vile nitapamba na Wilson, na kumuomba Shane aitunze familia yake, Marian na Joey iwapo atakufa. Shane, anatambua ya kwamba Starrett sio saizi yake kwa Wilson katika suala zima la kupigana kwa kutumia bunduki..anasema lazima niende mimi badala yake. Starrett anagoma, na Shane analazimika kumzimisha. Marian mwenye mashaka tele anamwuliza Shane kwanini anafanya anawasaidia. Kwa ajili yake, mumewe na mtoto wao na watu wote wenye busara wanaoishi katika bonde hilo wanaotaka nafasi ya kuishi kwa amani.
Wakati Shane akielekea mjini, Joey anamfuata kwa miguu. Huko baa, Shane anamweleza Ryker hawezi kushinda hili, kwa sababu tu wakati umebadilika; wezi wako wa ng'ombe na wapiganaji wako wamepitwa na wakati. Halafu anamgeukia Wilson: "Nimesikia habari kama huna lolote mwongo tu," anasema. "Thibitisha," anajibu Wilson, na kutoa bastola yake. Shane kamshinda kwa kutoa bastola haraka, kisha na kumpiga Ryker vilevile, wakati anajaribu kutoa bastola yake aliyoificha. Kabla ndugu yake Ryker, Morgan, aliyejificha dalini, kumtandika risasi ya mgongoni Shane, Joey anapiga ukelele wa onyo, na Shane anamwua Morgan vilevile.
Shane anamwambia Joey nenda nyumbani kamwambie mama yake ya kwamba wakazi wameshinda, ya kwamba hakuna tena mabunduki katika bonde hilo. Wakati Joey anamsogelea, matone ya damu yanammwagikia katika mkono wake wa kushoto; mkono wa kushoto wa Shane unaonekana kuwa na jelaha huku akipanda farasi wake. Katika tukio la mwisho la pekee, Shane anaondoka mjini pale, anasogeza mbele kitako chake cha farasi, huku akipuuzia kilio cha mvurugo cha Joey cha kumtaka "Shane! rudi!"
Waigizaji
[hariri | hariri chanzo]- Alan Ladd kama Shane
- Jean Arthur kamaMarian Starrett
- Van Heflin kama Joe Starrett
- Brandon deWilde kama Joey Starrett
- Jack Palance (humu katajwa kama kama Walter Jack Palance) kama Jack Wilson
- Ben Johnson kama Chris Calloway
- Edgar Buchanan kama Fred Lewis
- Emile Meyer kama Rufus Ryker
- Elisha Cook, Jr. kama Frank 'Stonewall' Torrey
- Douglas Spencer kama Axel 'Swede' Shipstead
- John Dierkes kama Morgan Ryker
- Ellen Corby kama Mrs. Liz Torrey
- Paul McVey kama Sam Grafton
- John Miller kama Will Atkey, bartender
- Edith Evanson kama Mrs. Shipstead
- Leonard Strong kama Ernie Wright
- Nancy Kulp kama Mrs. Howells
Athira kwa kazi za baadaye
[hariri | hariri chanzo]Sehemu kama "Come Back, Shame" na "It's How You Play the Game" katika mfululizo wa TV Batman uliomwonesha adui jina lake Shame, mwigo wa shujaa Shane.[7]
Katika filamu ya mwaka wa 2017 Logan imetoa maudhui ya kina juu ya athira kutoka kwa Shane, na kurejea maneno kadha wa kadha katika majibizano ya filamu hii katika vipande kadhaa. Wakati filamu inakwisha, maneno ya kwaheri ya Shane kwa Joey yanatajwa, maneno yaleyale, katika kabuli la Logan.[8]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Box Office Information for Shane. The Numbers. Retrieved April 13, 2012.
- ↑ Variety film review; April 15, 1953, page 6.
- ↑ Harrison's Reports film review; April 18, 1953, page 63.
- ↑ 4.0 4.1 Andrew, Geoff. "Shane", Time Out Film Guide, Time Out Guides Ltd., London, 2006.
- ↑ "Shane". Turner Classic Movies. Atlanta: Turner Broadcasting System (Time Warner). Iliwekwa mnamo Septemba 6, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Schaefer, Jack (1983). Shane (toleo la Paperback). New York City: Bantam Books. ISBN 978-0553271102.
- ↑ van Heerden 1998, p. 162.
- ↑ What was that Western Movie in Logan? Archived 14 Machi 2017 at the Wayback Machine. at geekendgladiators.com, retrieved March 13, 2017.
Vyanzo
[hariri | hariri chanzo]- Vermilye, Jerry (2012). Jean Arthur: A Biofilmography. Bloomington, Indiana: AuthorHouse. uk. 143. ISBN 978-1467043274.
- Hyams, Jay (1984). The Life and Times of the Western Movie (toleo la 1st). New York City: Gallery Books. ku. 115–116. ISBN 978-0831755454.
- Brady, Thomas F.. "Paramount Gets Option on Novel: to Enact Title Role", The New York Times, New York City: The New York Times Company, March 1, 1950, p. 42. Retrieved on September 6, 2016.
- Brady, Thomas F.. "Warners Acquire 'Winterset' Rights: Studio Buys Screen Privilege From R.K.O. and May Star Humphrey Bogart in It Of Local Origin", The New York Times, New York City: The New York Times Company, March 24, 1950, p. 29. Retrieved on September 6, 2016.
- NY Times Staff. "Alan Ladd to Star in Historical Film: He Will Appear in 'Quantrell's Raiders,' Which Wallis Will Produce at Paramount U.-I. Buys "Fifth Estate"", The New York Times, New York City: The New York Times Company, September 27, 1950, p. 48. Retrieved on September 6, 2016.
- van Heerden, Bill (1998). Film and Television In-Jokes: Nearly 2,000 Intentional References, Parodies, Allusions, Personal Touches, Cameos, Spoofs and Homages (toleo la Paperback). McFarland & Company. uk. 162. ISBN 978-1476612065.
Cliff Robertson appears as the villain Shame (a takeoff on Alan Ladd's western hero, Shane, 1953)
- Lev, Peter (2003). Transforming the Screen, 1950-1959. Oakland, California: University of California Press. uk. 116. ISBN 9780520249660.
Jisomee
[hariri | hariri chanzo]- Walt Farmer (2001). The Making of Shane in Jackson Hole, Wyoming. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-10. Iliwekwa mnamo 2017-04-23.
{{cite book}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) CD-ROM. - Slotkin, Richard (1992). "Killer Elite: The Cult of the Gunfighter, 1950–1953". Gunfighter Nation: The Myth of the Frontier in Twentieth-Century America. New York: HarperPerennial. ku. 379–404. ISBN 0-06-097575-X.
{{cite book}}
: External link in
(help); Unknown parameter|chapterurl=
|chapterurl=
ignored (|chapter-url=
suggested) (help)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Shane at the Internet Movie Database
- Shane at the TCM Movie Database
- Kigezo:Allmovie title
- Kigezo:AFI film
- Shane katika Rotten Tomatoes
- Shane at Filmsite.org