Nenda kwa yaliyomo

Seknidazoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Seknidazoli (Secnidazole), inayouzwa kwa jina la chapa Solosec miongoni mwa mengine, ni dawa ya kuua vijidudu inayotumika kutibu ugonjwa wa bakteria ya sehemu ya uke na maambukizi ya kijinsia yanayosababishwa na vimelea.[1][2] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maambukizi ya chachu ya uke, maumivu ya kichwa, kichefuchefu, kuhara, na maumivu ya tumbo.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha usalama wa matumizi yake katika ujauzito na unyonyeshaji yasiyo kuwa wazi.[1] Dawa hii ni nitroimidazole ambayo utaratibu wake wa utekelezaji haueleweki kabisa.[1]

Seknidazoli iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2017.[1] Nchini Marekani, dozi moja inagharimu takriban dola 280 za Marekani kufikia mwaka wa 2021.[3] Imekuwa hata hivyo ikipatikana katika sehemu nyingine za dunia kwa miongo kadhaa.[4]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Secnidazole Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 11 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. kumar, Sunesh; Padubidri, V. G.; Daftary, Shirish N. (24 Julai 2018). Howkins & Bourne, Shaw's Textbook of Gynecology, 17edition-EBOOK (kwa Kiingereza). Elsevier Health Sciences. uk. 365. ISBN 978-81-312-5412-7. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 11 Oktoba 2021.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Secnidazole Prices and Secnidazole Coupons - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 11 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Nyirjesy, P; Schwebke, JR (Aprili 2018). "Secnidazole: next-generation antimicrobial agent for bacterial vaginosis treatment". Future microbiology. 13: 507–524. doi:10.2217/fmb-2017-0270. PMID 29327947.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Seknidazoli kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.