Sarah Hunter

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sarah Alice Hunter

Sarah Alice Hunter,(alizaliwa mnamo 19 Septemba 1985) ni mchezaji wa timu ya taifa ya Raga Uingereza. Amewakilisha Uingereza tangu Kombe la Dunia la Raga ya Wanawake wa 2010 na sasa ni nahodha wa timu hiyo.[1]

Kazi ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Hunter aliichezea Uingereza kwa mara yake ya kwanza mwaka 2007 [2]. Alikuwa amefanya mafunzo kama kiungo lakini alijiunga na kikosi cha Uingereza kama mchezaji wa nyuma baada ya kocha Phil Forsyth kumhamisha katika majaribio ya Chini ya mara 19.

Yeye aliongoza timu Uingereza kushinda taji la 2014 Wanawake Raga Kombe la Dunia na alikuwa nahodha kwa mara ya mia moja mwezi Novemba 2017 ambapo Uingereza iilicheza thidi ya Canada katika nusu fainali ya 2017 a Raga ya Wanawake Kombe la Dunia. Mnamo Aprili 2021, Hunter ni mchezaji wa pili wa Uingereza anaengoza kwa kuwa nahodha mara nyingi zaidi ya wakati wote

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Hunter akiwa na miaka 15 alijiunga na Lichfield Ladies.Alihamia Bristol Ladies mnamo 2015 na baadae kujiunga na Loughborough Lightning mwaka 2017, ambapo ndipo anapochezea.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Hunter alizaliwa huko North Shields mwaka wa 1985. Alianza kucheza katika ligi ya raga akiwa na umri wa miaka 9 katika shule ya msingi ya Goathland, akichezea timu ya kina Longbenton na Gateshead Panthers.

Alisoma Sayansi ya Michezo na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Loughborough. Aliendelea kufanya kazi katika RFU kama Ofisi ya Maendeleo ya Raga ya Chuo Kikuu ya Kusini Magharibi.

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Hunter aliteuliwa kuwa Mwanachama wa Order ya Dola ya Uingereza ijulikanayo kama "Member of the Order of the British Empire (MBE)"</ref>[3]

mnamo 2015 huko New York. Alitajwa kuwa mchezaji bora wa Kombe la Dunia la Raga ya Wanawake mwaka 2016. [4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Hunter returns to captain England". Loughborough University (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-20. 
  2. "Hunter to win 100th cap for England", BBC Sport. (en-GB) 
  3. 2015 New Year Honours List
  4. "RFU". www.englandrugby.com. Iliwekwa mnamo 2021-04-20. 
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sarah Hunter kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.