Nenda kwa yaliyomo

Sara Hlupekile Longwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sara Hlupekile Longwe ni mshauri wa masuala ya jinsia na maendeleo Lusaka, Zambia. Alikuwa mwenyekiti wa FEMNET kati ya 1997 na 2003. Longwe ndiye mwandishi wa mfumo wa Longwe wa Uchambuzi wa jinsia. Longwe anajielezea kama mwanaharakati mwenye itikadi kali za kifeministi.