Sandra Arenas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sandra Lorena Arenas Campuzano (amezaliwa Pereira, Kolombia, Septemba 17, 1993) ni miongoni mwa wanariadha katika nchi hiyo.

Alishinda medali ya fedha katika mbio za kutembea kwa haraka za kilometa 20 za Olimpiki ya Msimu wa joto katika mwaka 2020 huko Tokyo. Pia alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Msimu wa joto wa mwaka 2012,mwezi wa tano huko Landani katika michezo hiyo alishiriki mbio za kilomita 20.

Pia alishiriki katika kombe la Dunia la IAAFla mwaka 2012 huko Saransk, Urusi alishinda mbio za kilomita 10 za wanawake, Mnamo Julai 2012, Arenas alishinda medali ya shaba katika mbio za kilomita 10 za Mashindano ya Dunia ya Wanariadha wa 2012 kwa muda wa 45:44.46. Arenas alishika nafasi ya 32 katika mbio za kutembea kwa haraka za kilomita 20 kwenye Olimpiki ya Msimu wa joto ya 2012 kwa muda wa 1:33:21. Alishika Nafasi ya 32 Tena kwenye Michezo ya Olimpiki ya Msimu wa joto wa 2016, kwa muda wa 1:35:40; Pia alishika nafasi ya Pili katika Michezo ya Olimpiki ya Msimu wa 2020, kwa muda wa 1:29:37.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]