Salvador Dali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Salvador Dali 1965
Dali 1944: "Ndoto iliyosababishwa na nyuki aliyezunguka tunda sekunde moja kabla ya kuamka"

Salvador Dalí (11 Mei 1904 - 23 Januari 1989) aliitwa kwa jina la kiraia Salvador Felipe Jacinto Dalí Domènech alikuwa mchoraji mashuhuri wa Hispania katika karne ya 20. Alifahamika zaidi kwa taswira zake katika mtindo wa usurealisti lakini alikuwa pia mwandishi, mchongaji na mwigaji wa maigizo.

Picha zake zilionyesha mara nyingi ndoto, malevi, homa na maono. Mara kwa mara alimwingiza mke wake Gala ndani ya taswira.

Kati ya wasanii muhimu wa Hispania wa karne ya 20 alikuwa mmoja wa wachache waliompenda dikteta Jenerali Francisco Franco. Alipingwa mara nyingi kwa msimmao huu wa kisiasa.

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons


Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Salvador Dali kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.