Ryan Reynolds

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ryan Reynolds
Ryan Reynolds

Ryan Rodney Reynolds (amezaliwa 23 Oktoba 1976) ni mwigizaji mwenye asili ya Kanada-Amerika anayejulikana kama Wade Wilson/Deadpool katika filamu ya Deadpool na Deadpool 2 na kama Michael Bryce katika The Hitman's Bodyguard. Pia anajulikana Kwa kucheza filamu kama, National Lampoon's Van Wilder, Just Friends, Definitely, Maybe, The Proposal, The Change-Up, Safe House, na Free Guy.

Reynolds aliigiza kama Detective Pikachu katika filamu ya 2019 Pokémon: Detective Pikachu. Reynolds pia aliigia kama Deadpool katika mfululizo wa Screen Junkies's .

Reynolds alizaliwa Vancouver, Columbia ya Uingereza. Alisoma Shule ya Sekondari Kitsilano na Chuo Kikuu cha Kwantlen Polytechnic. Reynolds alimuoa Scarlett Johansson na ndoa bio ilidumu kuanzia 2008 hadi 2011. Alimuoa Blake Lively na ndoa hio ilidumu kuanzia mwaka wa 2012 mpaka hivi sasa na kufanikiwa kupata watoto mabinti watatu. Mnamo Septemba 2022, ilitangazwa kuwa wenzi hao wanatarajia mtoto wao wa nne.

Reynolds alipokea nyota kwenye Hollywood Walk of Fame mwaka 2016.


Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ryan Reynolds kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.