Nenda kwa yaliyomo

Ruwaza ya Kenya 2030

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ruwaza ya Kenya 2030 (Kiingereza: Kenya Vision 2030) ni mpango wa maendeleo ya kiuchumi wa serikali ya Kenya kuendeleza maeneo mbalimbali ya kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi. Malengo ya mpango kuzalisha ukuaji wa uchumi wa mwaka wa 10%. Hivi sasa, Kenya ina ukuaji wa Pato la Taifa 4.9% (2007). Maono haya yamefululizwa katika miaka mitano mitano ya mipango, mwanzo wake ukiwa 2008-2012. Mpango wa kwanza unaazimia uwekezaji katika sekta sita muhimu na miradi ishirini kabambe. Sekta zilizolengwa ni pamoja na utalii, kilimo, viwanda, biashara, teknolojia ya habari, na huduma za kifedha.

Kulitangazwa 10 Juni 2008, kwamba wilaya ya Isiolo, itakuwa ya kwanza ya mradi wa kewekezwa. Mpango unazimia kuufanya mji wa Isiolo kuimarika kama eneo la kitalii ambalo litajumuisha kasino, mahoteli, masoko rejareja, uwanja wa ndege wa kisasa na vifaa vya usafiri.[1]

Serikali ya Kenya ilitangaza wakati wa 2008 Summer Michezo ya Olimpiki mjini Beijin ina mpango kabambe wa kuwa mwenyeji wa Micheza ya Olimpiki mwaka 2028 kam amojawapo ya mipanngo ya kutimiza ruwaza ya kenya 2030.

Maeneo ya mijini nchini Kenya itakuwa karibu maradufu kufikia mwaka 2030, na yatavujika na zaidi ya 2 / 3 ya idadi ya watu ambao watazingira maeneo ya mijini.

Serikali ya Kenya inatarajia kwamba mpango huu utaimarisha sekta ya utalii nchini Kenya. Hivi sasa, utalii umeegemea safari porini. Mpango huu unatoa wito kwa uwekezaji katika miji ya pwani.[2]

  1. Mburu, Solomon. "Isiolo on way to becoming leading tourist resort", Business Daily Africa, 10 Juni 2008. Retrieved on 2008-06-23. 
  2. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named Ratemo1

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ruwaza ya Kenya 2030 kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.