Ruth Pointer
Ruth Pointer (alizaliwa 19 Machi 1946[1] huko Oakland, California) ni mwanamuziki kutoka nchini Marekani. Anajulikana sana kwa kuwa mmoja wa kundi la The Pointer Sisters.[2] Kundi maarufu la muziki wa pop, R&B na soul.
Alianza safari ya muziki akiwa na dada zake akina Pointer Sisters. Ambao ni June na Bonnie Pointer, kabla ya Ruth kujiunga nao mwaka 1972. Ruth alikuwa na sauti nzito na yenye nguvu, ambayo iliongeza ladha katika muziki wa kundi hilo.
Pointer Sisters walipata umaarufu mkubwa katika miaka ya 1970 na 1980. Walitoa albamu nyingi zilizofanikiwa kibiashara. Baadhi ya albamu zao maarufu ni pamoja na "Energy" (1978), "Break Out" (1983), na "Contact" (1985).
Albamu hizi zilitoa nyimbo nyingi zilizopendwa na mashabiki, zikiwemo "Jump (For My Love)", "I'm So Excited", "Neutron Dance", na "Automatic". Nyimbo hizi zimekuwa sehemu ya utamaduni wa pop, na zinaendelea kupendwa hadi leo.
Kama mwanachama wa Pointer Sisters, Ruth Pointer amepata tuzo nyingi, ikiwa ni pamoja na tuzo za Grammy kwa nyimbo na albamu zao maarufu. Pointer Sisters walijulikana kwa mtindo wao wa ulioujumuisha aina anuwai za muziki kama vile rock, jazz, na disco. Licha ya mabadiliko ya mara kwa mara katika muziki na wanachama wa kundi hilo, Ruth Pointer amebaki kuwa kiungo muhimu na sauti inayoendelea kuvuma katika historia ya muziki wa kundi na Marekani kwa ujumla.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "The Pointer Sisters | Members, Songs, I'm So Excited, & Facts | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). 2024-07-05. Iliwekwa mnamo 2024-08-10.
- ↑ "Group Bio (Extended)". thepointersisters.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-08-10.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Pointer Ruth Pointer katika Discogs
- Ruth Pointer at the Internet Broadway Database
Makala hii ni sehemu ya mradi wa kuboresha Wikipedia na Wikamusi ya Kiswahili. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari. |