Nenda kwa yaliyomo

Rose Mukankomeje

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Rose Mukankomeje ni mwanasiasa, mwanabiolojia, na mwanaharakati wa mazingira wa Rwanda, ambaye kazi yake nikushughulikia uhifadhi wa misitu ya Rwanda.

Mukankomeje alihudumu kama mbunge wa bunge la Rwanda kuanzia 1995 hadi 2001. [1]

Mukankomeje aliwahi kuhudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa Rwandan Environment Management Authority (REMA).[2] Kazi yake ilisababisha Rwanda kushinda tuzo ya mwaka 2011 ya Future Policy Award kwa Sera ya Taifa ya Misitu, ambayo ilinukuu “mabadiliko makubwa katika mwelekeo wa kupungua kwa uoto wa misitu” nchini Rwanda.[1][3]

Mnamo mwaka 2013, Mukankomeje alipokea Forest Hero Award kutoka kwa United Nations Forum on Forests.[2] Tuzo hiyo ilitambua juhudi zake katika kuendeleza Umuganda, mradi wa kila mwezi wa upandaji miti unaohusisha jamii; kuhamasisha kilimo endelevu; na kazi yake katika utekelezaji wa marufuku ya kitaifa ya mifuko ya plastiki.[2]

Mukankomeje kama sehemu ya ujumbe wa Rwanda katika Mazungumzo ya Tabianchi ya Paris (COP21), 2015

Mnamo mwaka 2019, Mukankomeje aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa High Education Council (HEC) nchini Rwanda.[4]

  1. 1 2 "United Nations Forum on Forests » Africa". www.un.org (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-03-09.
  2. 1 2 3 "United Nations Forum on Forests » UNFF » One woman's heroic efforts to restore more than just Rwanda's forests". www.un.org (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-03-09.
  3. "Forest policies in Rwanda, United States and Gambia win UN-backed awards". UN News (kwa Kiingereza). 2011-09-21. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-01-20. Iliwekwa mnamo 2022-03-10.
  4. "Senate Powers to Confirm Officials Creates Heated Debate in Plenary". KT PRESS (kwa American English). 2019-11-14. Iliwekwa mnamo 2022-03-09.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rose Mukankomeje kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.