Rosa Luxemburg
Rosa Luxemburg (5 Machi 1871 - 15 Januari 1919) alikuwa mwanasiasa na mwanafalsafa kutoka Poland aliyeishi muda mrefu Ujerumani.
Alizaliwa katika familia ya Wayahudi katika sehemu ya Poland iliyokuwa sehemu ya milki ya Urusi. Tangu utoto alijiunga na vikundi vya kisoshalisti waliopinga utawala wa Kirusi. Alilazimishwa kukimbia akakaa Uswisi aliposoma falsafa, historia na uchumi. 1897 alimwoa Mjerumani akahamia Berlin aliposhiriki katika chama cha kisoshalisti SPD akawa mwalimu kwenye chuo cha chama.
Aliendeleza mafundisho ya Kimarx katika vyama vya kisoshalisti vya Ulaya. 1914 alipinga vita kuu ya kwanza ya dunia akajitenga na chama cha kisoshialisti cha Ujerumani baada ya wabunge wa chama hiki kukubali mikopo ya kulipia gharama za vita kwenye bunge la Ujerumani.
Rosa alikuwa kati ya waanzilishaji wa chama cha Kikoministi katika Ujerumani lakini wakati huohuo alipinga mweleko wa kidikteta kati ya Wakomunisti wa Urusi chini ya Lenin.
Baada ya mapinduzi ya Ujerumani ya 1918 yaliyomaliza utawala wa Kaisari aliendelea kupigania mapinduzi ya kisoshalisti. Wakati wa mgomo wa wafanyakazi Wakomunisti alikamatwa na vikosi vya wanamgambo waliopinga mapinduzi akauawa nao na maiti yake kutupwa mtoni.
Anakumbukwa kama mwanamapinduzi aliyependa uhuru. Kati ya misemo yake yanayokumbukwa ni "Uhuru wakati wote ni uhuru wa hao wasiokubaliana".
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rosa Luxemburg kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |