Romazava

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya mlo wa Romazawa
Picha ya mlo wa Romazawa

Romazava ([rumaˈzavə̥]) ni mlo wa kitaifa wa Madagaska, unaojumuisha mboga mboga, nyama ya zebu, nyanya, na vitunguu, kwa kawaida huambatana na sehemu ya wali. Sehemu muhimu ya kitoweo hicho ni brèdes mafana, iitwayo anamalaho katika Kimalagasi: Mmea huu una amidi ya asidi iitwayo Spilanthol katika vichipukizi vyake ambayo huleta athari ya kuchachusha, yenye ukali, ya machungwa na ya kufa ganzi, na kusababisha utowaji wa mate kupita kiasi.

=Marejeo[hariri | hariri chanzo]