Nenda kwa yaliyomo

Rolando José Álvarez Lagos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rolando José Álvarez Lagos

Rolando José Álvarez Lagos (alizaliwa 27 Novemba 1966) ni askofu wa Kanisa Katoliki kutoka Nikaragua. Tangu mwaka 2011, amekuwa Askofu wa Matagalpa na msimamizi wa kitume wa Estelí tangu mwaka 2021. Álvarez ni mpinzani wa muda mrefu wa Rais wa Nicaragua, Daniel Ortega.

Mnamo Februari 2023, baada ya kuzuiliwa kwenye kifungo cha nyumbani kwa miezi sita, alikataa kujiunga na kundi la wafungwa wejeoa kisiasa waliokabidhiwa kwa mamlaka ya Marekani. Baadaye alihukumiwa kifungo cha miaka 26 gerezani kwa kosa la usaliti. Mnamo Januari 2024, alifukuzwa nchini na kuhamishiwa Vatican City.[1]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.