Nenda kwa yaliyomo

Warohingya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Rohingya)
Bendera ya Warohingya.
Wakimbizi Warohingya mwaka 2012

Warohingya ni kundi lenye utamaduni wa Kiislamu katika Myanmar (Burma) ya magharibi linaloishi katika Dola la Rakhaing (Arakan) nchini Myanmar (Burma) hasa. Makundi mengine kutoka kwao wako pia nchini Bangla Desh. Wanaongea lugha ambalo ni karibu na Kichittagong na Kibengali.

Kwao nyumbani hawakubaliwi kama wazalendo iandaiwa ya kwamba walihamia hapa kutoka Bara Hindi hasa wakati wa Uhindi wa Kiingereza. Tangu 1983 waliondolewa uraia wa Burma. Kulikuwa na mawimbi ya mashambulio kutoka majirani yao ya Kiburma.

Mnamo mwaka 2013 takriban Rohingya 735,000 walikadiriwa wakiishi nchini Myanmar (Burma) hasa katika kaskazini ya mkoa na kwenye sehemu za pwani. Hapo ni asilimia 80-98 za wakazi. Zaidi ya milioni 1 wamekadiriwa kuishi nje ya nchi, wengi wakiwa wakimbizi.

Taasisi za kimataifa zimesema kuwa Warohingya wako kati ya vikundi wa watu wanaoteswa zaidi duniani.[1]

Mwaka wa 2015, hali ya kusikitisha ya wakimbizi Warohingya kwenye bahari ya Kihindi iliripotiwa kipana na vyombo vya habari vya kimataifa.

  1. "Kuihusu hali ya Warohingya katika Bangladesh". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-19. Iliwekwa mnamo 2015-05-17.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Kujisomea

[hariri | hariri chanzo]