Roboti la mazungumzo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
ELIZA, roboti la mazungumzo lililoundwa mwaka 1966, lilifanikiwa kuwahadaa watu kuamini kuwa wanazungumza na binadamu kweli

Roboti la mazungumzo au roboti mazungumzo (kwa Kiingereza: chatbot, conversational robot au chatterbot) ni programu ya kompyuta inayoiga mazungumzo ya binadamu kwa njia ya maandishi au sauti. JapokuWa sio kila roboti la mazungumzo linatumia akili bandia, roboti nyingi za mazungumzo kwa sasa zinatumia usindikaji wa lugha ya asili kuelewa swali la mtumiaji na kuzalisha jibu lake.

Roboti mazungumzo hurahisisha utafutaji taarifa kwa kujibu haraka maswali na maombi ya watumiaji kwa njia ya maandishi, sauti au vyote.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "What is a chatbot? | IBM". www.ibm.com (kwa en-us). Iliwekwa mnamo 2024-01-11. 
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.