Robert Sithole

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Robert Sithole, alizaliwa mwaka 1945 alikuwa mwanamuziki wa Afrika Kusini.

Asili[hariri | hariri chanzo]

Sithole alizaliwa, na kukulia, katika Wilaya ya Sita, jumuiya iliyokuwa hai na yenye watu wengi huko Cape Town. Sithole aliondolewa Rylands kutokana na kipindi cha ubaguzi wa rangi na uharibifu wa Wilaya ya Sita.[1] Kwa muda, aliishi uhamishoni [[Uingereza].[2] Akiwa nchini Uingereza alihudhuria sherehe ya maadhimisho ya miaka 150 ya Robert Clarke, mtengenezaji wa filimbi ya Clarke, katika kijiji cha Suffolk cha Coney Weston mnamo Juni 1993, ambapo alicheza kwenye jukwaa pamoja na Mary Bergin na Bill Ochs.

Ushawishi wa muziki na Kazi[hariri | hariri chanzo]

Sithole alikuwa mmoja wa wakilishi bora wa filimbi,[2] muziki wake ukipata msukumo kutoka katika mitindo ya kwela na mbaqanga. Mwanzoni mwa kazi yake alicheza na Kwela Kids huko Cape Town na baadaye na Sipho Mabuse katika Beaters huko Johannesburg. Ujuzi wa Sithole kama mwanamuziki haukuleta mafanikio ya kifedha hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 1990 alikuwa hana mafanikio, akaanza uimbaji wa mitaani katika mitaa ya Cape Town. Alifanya kwa muda kama mwanamuziki mkazi katika Makumbusho ya Wilaya Sita huko Cape Town, na hivyo kuishia kuwa na afya dhoofu iliyoathiriwa na uvutaji sigara, afya yake ilipungua kwa kasi.

Alifariki mnamo tarehe 7 Juni mwaka 2006, alifariki akiwa na umri wa miaka 61.

Urithi[hariri | hariri chanzo]

Muziki wake unaonekana kwenye Images of Africa (vol. 12) ya mwaka 2000. Sithole alikuwa, pamoja na kaka yake Joshua, pia mwanamuziki, alikuwa katika uchoraji wa filimbi kwa Vladimir Tretchikoff.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Beyond the Blues: Township Jazz in the '60s and '70s (kwa Kiingereza). New Africa Books. 1997. ISBN 9780864862426. 
  2. 2.0 2.1 Halperin, Ian (2015-06-09). Whitney and Bobbi Kristina (kwa Kiingereza). Simon and Schuster. ISBN 9781501120749.