Rob Holding

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rob Holding

Rob Holding (alizaliwa 20 Septemba 1995) ni mchezaji wa soka wa Uingereza ambaye anacheza kama beki wa klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza iitwayo Arsenal.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Alianza kucheza akiwa na klabu ya Bolton Wanderers, na alianza kucheza rasmi mwezi Aprili 2015 wakati akiwa kwa mkopo huko Bury. Baada ya msimu mmoja katika timu hiyo ya Bolton, alijiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza iitwayo Arsenal mnamo Julai 2016.Akiwa na klabu ya Arsenal alishinda Kombe la FA na FA Community Shield.

Kazi ya kkimataifa[hariri | hariri chanzo]

Holding amewakilisha Timu ya taifa ya Uingereza chini ya umri wa miaka 21 na alikuwa sehemu ya timu iliyoshinda mashindano ya Toulon mwaka 2016.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rob Holding kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.