Rhino Ark

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Rhino Ark ni shirika la hisani nchini Kenya linalolenga kukusanya pesa kwa kujenga fensi ya kuzunguka Aberdares National Park na Aberdares Conservation Area penye makazi ya vifaru walio hatarini ya kutoweka kutokana na uwindaji usio halali.

Shabaha ya shirika ni kuzuia matumizi yasiyo halali ya misitu ya Aberdares na kusaidia matumizi endelevu ya msitu na mazao yake kwa manufaa ya watu wanaoishi kando la Aberdares.

Fensi ya Aberdares ilikamilika mwezi wa Agosti 2009 [1]

Kila mwaka kuna mashindano ya magari ya Rhino Charge yanayolenga kukusanya pesa kwa ajili ya Rhino Ark.

Kuna pia tawi la shirika huko Uingereza wanakofanya pia mashindano ya kukimbia magari.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Daily Nation, August 29, 2009: Fencing of Aberdares completed

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]