Rhino Charge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Rhino Charge 2007
Rhino Charge Action

Rhino Charge ni tukio la kila mwaka, linalifanyika nchini Kenya, ambalo washindani wana kushindana kwenye njia mbaya wakitumia magari ya aina ya 4x4. Fedha zote zinazokusanywa hupewa chama cha Rhino Ark, ambacho husaidia kuhifadhi eneo la Aberdare. Washindani hutakiwa kulipa kiwango cha chini zaidi ya pesa za udhamini lakini kuna timu ambazo hupitisha kiwango hiki, rekodi iliyopo hadi sasa ni shilingi 9,393,552 na iliwekwa na timu ya gari nambari 5 ya Alan McKittrick, Bruce Knight, Charlie Hewitt-Stubbs, John Trundell, S. McKittrick, washindi wa tuzo lililodhaminiwa sana la David Schaeffer. Wadhamini wa muda mrefu kama Mike and Sarah Higgins wamekusanya shilingi 39,604,399 katika muda wa miaka 20.

Washindani wanafaa kupitia pointi 13 zilizosambaratika katika eneo la kama mita 100 kwa mita 100 lililo na ardhi mbovu sana wakitumia masaa 10 pekee. Washindani hupewa mapu iliyo na skeli ya 1:50,000 ya eneo hilo, pointi hizo 13 na pale watakapoanzia. Kila mshindani hufuata njia yake na mshindi ni yule atakayepitia pointi zaidi na muda mfupi zaidi

Kwa ajili ya mazingira, tukio hili huwa na magari yasiyopita 60.

Tukio hili ni sawa ni lingine linalifanyika kila mwaka mjini Sussex, Marekani Matukio mengine yanayofanyika kusaidia 'Rhino Ark' ni 'Quattro Charge' na 'Hog Charge' ambalo ni la watoto wakitumia baiskeli.

Maandiko ya Chini[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Flag-map of Kenya.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rhino Charge kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.