Rasi Agulhas
Mandhari
Rasi Agulhas (ing. Cape Agulhas) ni mahali pa kusini zaidi pa bara la Afrika. Iko karibu na mji wa Agulhas katika Afrika Kusini. Iko karibu pia na Rasi ya Tumaini Jema iliyo maarufu zaidi.
Ni mpaka kati ya maji za Atlantiki na Bahari Hindi na mstari unaoelekea kusini kutoka hapa umekubaliwa na Shirika la Kimataifa la Hidrografia kuwa mpaka kati ya bahari hizi mbili.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Agulhas National Park Archived 27 Januari 2011 at the Wayback Machine.
- Cape Agulhas
- Travel to Cape Agulhas