Ramiro Corrales

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramiro Corrales
Naibu nahodha wa San Jose Earthquakes,Ramiro Corrales
Maelezo binafsi
Jina kamili Ramiro Corrales
Tarehe ya kuzaliwa 12 Machi 1977
Mahala pa kuzaliwa    Salinas,California, Marekani
Urefu 6ft
Nafasi anayochezea Difenda
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa San Jose Earthquakes
Namba 12
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
1995
1996
1996–1997
1997–1998
1998–2001
2001–2004
2005–2006
2007
2008–
California Jaguars
Columbus Crew
San Jose Clash
Miami Fusion
MetroStars
San Jose Earthquakes
Hamarkameratene
Brann
San Jose Earthquakes
Timu ya taifa
1996–2008 Marekani

* Magoli alioshinda

Ramiro Corrales (alizaliwa Salinas, California, 12 Machi 1977) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Marekani.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Klabu[hariri | hariri chanzo]

Corrales hakucheza soka akiwa chuo kikuu, bali alitia saini mkataba na timu ya California Jaguars wa ligi ya USISL. Alianza kucheza kama mchezaji bora na akorodheshwa katika Orodha ya 1996 Ligi Kuu ya Soka ya Marekani. Hii ilikuwa kabla kuja kwa Project-40,hivyo basi Corrales akaacha nafasi ya kupewa udhamini wa kusoma katika chuo kikuu. Corrales aliorodheshwa kama # 81 na timu ya Columbus Crew lakini akauzwa mara iyo hiyo kwa timu ya San Jose Clash (iliyokuja kuitwa "Earthquakes" baadaye) katika mkondo wa pili wa uchaguzi katika orodha ya wachezaji wa Ligi Kuu ya Soka ya Marekani.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa San Jose Clash,alifunga bao moja na kusaidia katika kufungwa kwa bao jingine katika mechi 11 alizocheza. Alianza katika mechi 11 katika msimu uliofuata. Mnamo Novemba 1997, Corrales aliorodheshwa katika # 16 na timu ya Miami Fusion katika Orodha ya Wachezaji iliyopanuliwa ya 1997.Aliuzwa tena Juni 1998,wakati huu kwa timu ya MetroStars akibadilishwa na Carlos Parra. Akiwa katika timu ya Metros, Corrales mchezaji wa pili aliyecheza dakika nyingi zaidi katika timu,katika mwaka wa 1999.

Katika mwaka wa 2001, Corrales alirudi tena San Jose huku Metros wakipata haki za kumtumia Paul Grafer. Alikuwa kiungo muhimu katika timu ya Frank Yallop iliyoshinda Kombe la Ligi Kuu ya Soka ya Marekani hapo 2001 na 2003. Katika miaka tisa akiwa Ligi Kuu ya Soka ya Marekani, Corrales amefunga mabao tisa na kusaidia katika kufunga kwa mabao 19. Corrales alikuwa mchezaji mzuri sana mwenye kipawa akiwa na uwezo wa kucheza nyuma,upande wa kushoto wa kati na upande wa kati katika timu.

Baada ya msimu wa 2004, Corrales alitia saini mkataba na klabu ya Unorwe, Hamarkameratene ambapo alicheza hasa kama mchezaji wa kushoto na nyuma. Alichaguliwa kama mchezaji bora wa mwaka katika klabu katika msimu wa 2006 katika gazeti la Hamar Arbeiderblad na pia na mashabiki katika tovuti ya klabu yake.

5 Januari 2007, Hamarkameratene na timu ya Brann walikubaliana katika mkataba wa uhamisho lakini lakini Corrales alifukuzwa Unorwe tarehe 9 Februari na Bodi ya Kinorwe ya Uhamiaji, hii ikatishia kuharibu mpango wa kuchezea Brann. Corrales alifukuzwa kwa sababu alikuwa amecheza msimu mzima wa 2006 bila kibali cha kufanya kazi huko. [6] Kesi ilitatuliwa tarehe 14 Machi, bodi ya Unorwe ya Uhamiaji ikampa Corrales kibali kipya cha kazi.

Baada ya mechi ya Marekani dhidi ya Uswidi, Ramiro alikataa kurudi Bergen na akawasilisha kuwa heri angeacha kucheza soka badla ya kurudi huko. Alidai kuwa hali ya anga ya Bergen haikuwa nzuri kwake, lakini baadaye alisema angeweza kukubali uhamisho kuenda Oslo ambako kuna hali ya anga iliyokauka kuliko Bergen. Yeye pia alisema hapendi kukalishwa kwenye benchi badala ya kuchezeshwa.

Corrales hatimaye alirejea Marekani katika mwaka wa 2008, akitia saini mkataba na timu ya San Jose Earthquakes.

Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Ramiro amechezea timu ya taifa ya Marekani ,akicheza katika daraja la vijana walio chini ya umri wa miaka 20 na daraja la vijana walio chini ya umri wa miaka 23. Alicheza ,pia,katika timu ya taifa katika mechi nne. Hii ilikuwa katika miaka ya 1990s,mara yake ya kwanza ilikuwa 16 Oktoba 1996 dhidi ya Peru). Yeye alicheza katika mechi mbili ya michezo ya Olimpiki ya 2000,akisaidia Marekani kufika nusu fainali. Alipewa nafasi katika timu ya taifa katika mwaka wa 2008 baada ya kuwa nje kwa miaka minane.

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Marekani[hariri | hariri chanzo]

  • Kombe la Ligi Kuu ya Soka ya Marekani: 2001 & 2003

Unorwe[hariri | hariri chanzo]

  • Ligi Kuu ya Soka ya Unorwe: 2007

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ "Ramiro årets spiller (Lugha ya Unorwe)". hamkam.no. 22 Aprili 2007. http://www.hamkam.no/presentation/showdetail.asp?id=4323 Archived Septemba 27, 2007 at the Wayback Machine..
  2. ^ "Brann kaprer Corrales (Lugha ya Unorwe)". brann.no. 22 Aprili 2007. http://www.brann.no/index.php?valg=nyhet&nyhet=5171 Archived Septemba 27, 2007 at the Wayback Machine..
  3. ^ "Ramiro Corrales kan glippe for Brann (Lugha ya Unorwe)". bt.no. 22 Aprili 2007. http://fotball.bt.no/eliteserien/article74694.ece Archived Septemba 27, 2007 at the Wayback Machine..
  4. ^ "Corrales blir spilleklar (Lugha ya Unorwe)". bt.no. 22 Aprili 2007. http://fotball.bt.no/eliteserien/article76814.ece Archived Machi 17, 2007 at the Wayback Machine..
  5. ^ Nettavisen - Visste ikke om ny lagkamerat [1]
  6. ^ [2]
  7. ^ [3] Archived Februari 11, 2008 at the Wayback Machine.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]