Nenda kwa yaliyomo

Rama Yade

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramatoulaye Yade-Zimet
Rama Yade 2007
Rama Yade 2007
Waziri msaidizi wa mambo ya nje
Tarehe ya kuzaliwa 13 Desemba 1976
Mahali pa kuzaliwa Dakar (Senegal)
Chama UMP
Dini Uislamu
Elimu yake Institut d’études politiques de Paris (IEP)
Digrii anazoshika Diploma (ya Kifaransa yalingana na MA)
Kazi 2000 utawala wa bunge (senati); 2007 serikali ya rais Sarkozy


Rama Yade (* 13 Desemba 1976) ni waziri msaidizi wa mambo ya nje katika serikali ya rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa.

Jina lake kamili ni Ramatoulaye Yade-Zimet. Alizaliwa nchini Senegal kama mtoto wa baba mwanasiasa Msenegal na mama aliyekuwa profesa wa chuo kikuu. Alihamia Ufaransa alipokuwa na umri wa miaka minane pamoja na familia wakati baba alikuwa mbalozi wa Senegal huko Paris. Wazazi waliachana na Rama alibaki na mama Ufaransa na kuchukua uraia huko.

Alisoma kwenye chuo cha Institut d'études politiques akamaliza kwa digrii ya diploma. Ajira yake ilipatikana katika utawala wa bunge la senati ya Ufaransa. Akajiunga na siasa ya chama cha UMP cha rais Jaques Chirac.

Baada ya kutoa hotuba kwenye mkutano wa kitaifa wa chama hiki mwaka 2006 alialikwa na mgombea wa urais Nicholas Sarkozy kujiunga na kampeni yake. Baada ya ushindi wa Sarkozy alikuwa waziri msaidizi wa mambo ya nje chini ya waziri Kouchner. Idara yake ni haki za binadamu katika siasa ya nje.

Ameolewa na Joseph Zimet ambaye ni mtumishi wa serikali na mwana wa mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za Kiyidish.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]