Raksibakumabi
Raksibakumabi (Raxibacumab) ni dawa inayotumika kutibu na kuzuia kimeta kilichovutwa katika pumzi.[1] Kwa ujumla, hutumiwa pamoja na dawa zinazotumika kutibu au kuzuia maambukizi ya bakteria (antibiotics).[1] Dawa hii inatolewa kwa sindano ya taratibu kwenye mshipa.[2]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu kwenye mahali pa sindano, maumivu ya kichwa, upele, kuwashwa na kuhisi usingizi.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha mzio mkali unaoweza kutishia maisha (anaphylaxis).[1] Ni kingamwili ya monokloni ambayo hufungamana na sehemu ya sumu ya Bacillus anthracis.[2]
Raksibakumabi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2012.[1] Katika Ulaya, ilipewa jina la yatima mwaka wa 2014.[3] Nchini Marekani, inaweza kununuliwa kutoka kwa Hifadhi ya Kitaifa ya Kimkakati.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "DailyMed - RAXIBACUMAB injection". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"DailyMed - RAXIBACUMAB injection". dailymed.nlm.nih.gov. Archived from the original on 19 March 2021. Retrieved 16 October 2021. - ↑ 2.0 2.1 "Raxibacumab Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"Raxibacumab Monograph for Professionals". Drugs.com. Retrieved 16 October 2021. - ↑ "EU/3/14/1352: Orphan designation for the treatment of inhalation anthrax disease". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Bower, William A. (0019). "Use of Anthrax Vaccine in the United States: Recommendations of the Advisory Committee on Immunization Practices, 2019". MMWR. Recommendations and Reports (kwa American English). 68. doi:10.15585/mmwr.rr6804a1. ISSN 1057-5987. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 August 2021. Iliwekwa mnamo 16 October 2021.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Raksibakumabi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |