Rai Benjamin
Mandhari
Rai Benjamin (amezaliwa Julai 27, 1997) ni mtaalamu wa kuruka viunzi na mwanariadha wa Marekani aliyebobea katika kuruka viunzi vya mita 400 na mbio za mita 400. Ni mtu wa pili kwa kasi ya kuruka viunzi vya miota 400 kwenye historia akiwa na rekodi binafsi ya muda wa sekunde 46.17. Alishinda medali ya fedha kwenye michezo yake ya kwanza ya olimpiki mwaka 2021 na katika michuano ya dunia ya mwaka 2019 kwenye kuruka viunzi kwa wanaume mita 400 na alishinda medali ya dhahabu kwenye mbio za kupokezana vijiti za mita 4 x 400 katika mashindano hayo.