Pyinmana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Pyinmana
Nchi Myanmar
Mahali pa Pinyama nchini Myanmar.

Pyinmana ni mji mdogo katika Myanmar karibu na Mandalay. Pia huitwa Naypyidaw, maana yake "Makao ya Wafalme". Mwaka 2005 serikali ya kijeshi iliamua kuhamisha mji mkuu kutoka Yangon kuja Pyinmana.

Pyinmana ilikuwa makao makuu ya "Jeshi la Uhuru wa Burma" wakati wa ukoloni na vita kuu ya pili ya dunia. Kwa wanajeshi wengi wa nchi ni kama mahali patakatifu.

Ilitajwa kama faida ya kuwa Pyinmana iko karibu zaidi na kitovu cha nchi kuliko Yangon (Rangun) ambayo iko kando. Sababu nyingine inayotajwa na wapinzani wa serikali ni ya kwamba ofisi za serikali ziko sasa mbali na watu wa Yangon walioandamana mara kwa mara na kudai demokrasia.

Map of Asian states.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Pyinmana kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: