Naypyidaw

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Pinyama nchini Myanmar.

Naypyidaw, maana yake "Makao ya Wafalme", awali: Pyinmana, ni mji wa tatu katika Myanmar karibu na Mandalay. Tangu mwaka 2005 ni mji mkuu wa nchi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Pyinmana ilikuwa makao makuu ya "Jeshi la Uhuru wa Burma" wakati wa ukoloni na vita kuu ya pili ya dunia. Kwa wanajeshi wengi wa nchi ni kama mahali patakatifu.

Mwaka 2005 serikali ya kijeshi iliamua kuhamisha mji mkuu kutoka Yangon kuja Pyinmana.

Ilitajwa kama faida ya kuwa Pyinmana iko karibu zaidi na kitovu cha nchi kuliko Yangon (Rangun) ambayo iko kando.

Sababu nyingine inayotajwa na wapinzani wa serikali ni kwamba ofisi za serikali ziko sasa mbali na watu wa Yangon walioandamana mara kwa mara na kudai demokrasia.

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Naypyidaw kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.