Programu ya kuendeleza ujasiriamali kwa vijana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Programu ya kuendeleza ujasiriamali kwa vijana ni jitihada zilizowekwa na Benki ya viwanda ili kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini Nigeria kwa kugharamia biashara mbalimbali zinazoanzishwa na vijana.

Programu hii ilijikita katika kuwapa vijana hao mbinu na ujuzi ili waweze kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha na kuendesha biashara zao wenyewe. Washiriki hutokea kati ya vijana wajasiriamali kati ya miaka 18 - 35 wenye wazo la biashara na Wenye kiwango cha elimu cha stashahada. [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "StackPath". www.boi.ng. Iliwekwa mnamo 2022-12-11.