Programming paradigm

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Programming paradigm ni jumla ya mawazo na dhana zinazoainisha mtindo wa kutengeneza programu za kompyuta.

Programming paradigm haiainishwi na lugha ya kutengeneza programu za kompuyta (programming language) tu. Karibu na lugha zote za kutengeneza programu za kompuyta za kisasa zinakubalia matumizi ya paradigms mbalimbali. Kwa mfano lugha ya C isiyo object-oriented inakubalia kutumiwa kufuatana na kanuni za object-oriented programming ingawa itakuwa na matatizo kadhaa. Functional programming inawezekana kutumiwa katika lugha yo yote ya imperative inayo functions na kadhalika.

Historia ya istilahi[hariri | hariri chanzo]

Istilahi “paradigm” kwa maana ya sayansi na teknolojia ya kisasa ilionekana kwenye kitabu cha Thomas Kuhn kinachoitwa Muundo wa mapinduzi ya teknolojia (The Structure of Scientific Revolutions) mwaka 1962 mara ya kwanza. Kuhn alitumia neno la paradigm kwa maana ya mifumo imara ya maoni ya kisayansi uchunguzi uliofanyiwa ndani yao. Kwa mujibu wa Kuhn wakati wa maendeleo ya taaluma ya kisayansi paradigm moja inaweza kubadiliwa na nyingine (kwa mfano Ptolemy alieleza muundo wa ulimwengu kwa kusema kuwa jua linazunguka dunia na paradigm hiyo ilibadilishwa na paradigm cha Copernicus aliyesema kuwa dunia linazunguka jua) ijapo paradigm ya kale inaendelea kuwa muda fulani na hata kusitawi kwa sababu wafuasi wake wengi hawawezi kufanya kazi kufuatana na paradimg niyingine kwa sababu hii au ile.

Istilahi hiyo ilitumiwa na Robert W Floyd wakati wa hotuba yake ya mwenye tunzo wa Turing Award.[1]

Floyd anazingatia kwamba katika kompuyta programming inawezekana kuona tokeo linalofanana na paradigms za Kuhn lakini kwa kutofautiana navyo programming paradigms hazitengani.

Ikiwa maendeleo ya ustadi wa kompyta programming kwa jumla yanahitaji uvumbuzi na uendelezaji wa paradigms wa kudumu maendeleo ya ustadi wa mtengeneza programu mmoja yanahitaji aongeze idadi ya paradigms alizo nazo.

Kwa hiyo kufuatana na Robert W Floyd kutofautiana na paradigms za kisayansi zilizoelezwa na Kuhn programming paradigms zinaweza kutangamana zikiongeza idadi yao mtengeneza programu anayodhibiti.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]