Nenda kwa yaliyomo

Paradigma ya programu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Paradigma ya programu ni jumla ya mawazo na dhana zinazoainisha mtindo wa kutengeneza programu za kompyuta.

Paradigma ya programu haiainishwi na lugha ya programu tu. Karibu lugha zote za programu za kisasa zinakubali matumizi ya paradigma mbalimbali. Kwa mfano lugha ya C isiyo inaozingatiwa kuhusu kipengee inakubali kutumiwa kufuatana na kanuni za paradigma inaozingatiwa kuhusu kipengee, ingawa kwa matatizo kadhaa. Functional paradigm inawezekana kutumiwa katika lugha yoyote ya imperative inayo functions na kadhalika.

Historia ya istilahi[hariri | hariri chanzo]

Istilahi “paradigma” kwa maana ya sayansi na teknolojia ya kisasa ilionekana mara ya kwanza katika kitabu cha Thomas Kuhn kinachoitwa Muundo wa mapinduzi ya teknolojia (The Structure of Scientific Revolutions) mwaka 1962. Kuhn alitumia neno paradigma kwa maana ya mifumo imara ya maoni ya kisayansi uchunguzi uliofanyiwa ndani yake. Kwa mujibu wa Kuhn wakati wa maendeleo ya taaluma ya kisayansi paradigma moja inaweza kubadiliwa na nyingine (kwa mfano Ptolemy alieleza muundo wa ulimwengu kwa kusema jua linazunguka dunia na paradigma hiyo ilibadilishwa na paradigma ya Copernicus aliyesema dunia linazunguka jua) ijapo paradigma ya kale inaendelea kwa muda fulani na hata kusitawi kwa sababu wafuasi wake wengi hawawezi kufanya kazi kufuatana na paradigma nyingine kwa sababu hii au hii.

Istilahi hiyo ilitumiwa na Robert W. Floyd wakati wa hotuba yake ya mwenye tuzo ya Turing Award.[1] Floyd anazingatia kwamba katika kompyuta programming inawezekana kuona tokeo linalofanana na paradigma za Kuhn lakini kwa kutofautiana navyo paradigma za programu hazitengani.

Ikiwa maendeleo ya ustadi wa kompyuta programming kwa jumla yanahitaji uvumbuzi na uendelezaji wa paradigma za kudumu maendeleo ya ustadi wa mtengeneza programu mmoja yanahitaji aongeze idadi ya paradigma alizonazo.

Kwa hiyo kufuatana na Robert W Floyd kutofautiana na paradigms za kisayansi zilizoelezwa na Kuhn programming paradigms zinaweza kutangamana zikiongeza idadi yao mtengeneza programu anayodhibiti.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.