Priscilla Misihairabwi-Mushonga
Priscilla Misihairabwi-Mushonga ni mwanasiasa wa Zimbabwe na balozi wa ufalme wa Sweden. Wakati akiwa mbunge wa Glen Norah pia aliwahi kuwa waziri kivuli wa mambo ya nje wa Movement for Democractic Change-Tsvangirai|Movement for Democratic Change. Wakati chama kilipogawanyika mwaka 2005, alibaki na MDC na alichaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho. Amekuwa akiwakilisha chama chake katika mazungumzo ya kisiasa ya Zimbabwe.
Kazi ya kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2009 aliteuliwa kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa. Katika serikali ya umoja wa kitaifa katika mkutano wa MDC wa 2011 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama, nafasi amabayo ataishikilia hadi mkutano ujao 2016. Ni mwakilishi mkuu wa MDC katika JJOMIC 9Kamati ya Pamoja ya Ufuatiliaji na Utekelezaji) na COPAC, kamati ya Bunge la katiba, kamati inayo husika na kuandika katiba ya Zimbabwe.[1]
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Alikuwa mjane baada ya mumewe, Dk Christopher Mushonga kufariki kutokana na majeraha aliyopata wakati wa wizi uliokosa kufaulu.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Cabinet sworn in amid chaotic scenes". NewZimbabwe.com. 13 Februari 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Februari 2009. Iliwekwa mnamo 2009-02-13.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Mushonga killer gang now faces murder charge", ZimDaily.com, 19 August 2009. Retrieved on 2024-09-28. Archived from the original on 2009-08-22.