Nenda kwa yaliyomo

Prajasakti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Prajasakti
Jina la gazeti Prajasakti
Aina ya gazeti *. Gazeti la kila siku
Lilianzishwa 1942
Eneo la kuchapishwa Maeneo ya Uhindi
Hyderabad, Vijayawada, Visakhapatnam, Tirupati (mji)
Khammam, Kurnool, Rajahmundry, Srikakulam ,Karimnaga
Nchi Uhindi
Mhariri *. S. Vinay Kumar (mhariri)
*. V. Krishnaiah (meneja mkuu)
Makao Makuu ya kampuni Hyderabad
Tovuti Tovuti rasmi ya Prajasakti

Prajasakti ni gazeti la lugha ya Kitelugu linalochapishwa kutoka Andhra Pradesh, Uhindi. Lilianza kama gazeti la kila siku katika mwaka wa 1981 , Vijayawada ikiwa makao lake. Hivi sasa, linachapishwa katika vituo 9 ( au matoleo) haswa Hyderabad, Vijayawada, Visakhapatnam, Tirupati (mji), Khammam, Kurnool, Rajahmundry, Srikakulam na Karimnaga. Liko na mtandao mpana wa kupata habari wa zaidi ya vituo 100 vya kukusanya habari katika jiimbo. Prajasakti limekua haraka sana na ,hivi sasa, ndilo gazeti la kila siku la Telugu linalosambazwa kabisa kuliko magazeti mengine ya Telugu. Katika mwaka wa 20 wa gazeti la Prajasakti,lilianzisha tovuti yao kwenye mtandao wa tarakilishi na kulifanya gazeti hili kuweza kufikia watu wote duniani.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Prajasakti lilianzishwa kama matunda ya mapambano ya uhuru. Lilianzishwa katika mwaka wa 1942 na likachapishwa kama gazeti la kila siku kutoka mwaka wa 1945. Baada ya kuanza tu, lilikandamizwa na Waingereza na likapigwa marufuku katika mwaka wa 1948. Lilianza kazi tena kama jarida la kila wiki katika mwaka wa 1969 na likakuwa gazeti la kila siku tangu mwaka wa 1981 huku Vijayawada ikifanywa kuwa kituo cha uhariri. Gazeti hili lilikuwa haraka sana katika miongo iliyofuata na likavutia nyoyo za raia , wafanyikazi na watu wa uwezo wastani wa kiuchumi. Prajasakti liliendelea mbele katika nyakati ambazo maendeleo na dhana ya demokrasia ilikuwa ikipingana na ubeberu. Toleo la pili lilianza katika mwaka wa 1997 katika Hyderbad, toleo la pili likaanzishwa pia katika mwaka wa 1997 katika Visakhapatnam, la nne katika mwaka wa 2001 katika Tirupati, la tano mnamo Julai 2003 katika Khammam, na la sita katika Kurnool mnamo Novemba 2003, la saba mnamo Mei 2005 katika Rajahmundry , la nane katika Karimnagar mnamo Septemba 2005 na la tisa katika Srikakulam katika mwaka wa 2006.

Prajasakti hulenga kufanya huru watu waliokandamizwa. Kutoka mwanzo wake wa 1981, lilikuwa azimio na mapambano ya wakulima. Prajasakti limeongoza daima katika kupigania sera za maendeleo na maadili mema katika jamii. Hupigania maadiili ya kidemokrasia, haki za wananchi wanaofanya kazi na huhimiza mapambano ya demokrasia dhidi ya sera za kibeberu zinazotumika duniani kote. Hufanya uchambuzi wa kisayansi katika masuala ya kisasa ,kimataifa na kitaifa. Prajasakti huunga mkono maadili ya haki na hupigania ,bila kuchoka,sera za kunyanyasa watu, ufisadi na masuala mengine mengi yanayofanya maisha ya maskini kuwa ngumu zaidi.

Wachapishaji na wafanyikazi

[hariri | hariri chanzo]

Prajasakti ni sehemu ya Prajasakti Sahithee Samastha ambayo ina makao yake makuu katika Hyderabad. Lina timu imara linalofanya kazi na mamia ya waandishi na wataalamu katika idara za matangazo, usambazaji, ufundi za teknolojia na bodi ya uhariri. Timu inaongozwa na S. Vinay Kumar akiwa mhariri na V. Krishnaiah akiwa meneja mkuu. Prajasakti lina chapishwa katika mitambo ya kuchapisha ya Prajasakti. Gazeti la Prajasakti hupeana msaada kwa kampuni za Prajasakti Book House na Prajasakti Publishing House ambazo ni vituo vya kuendeleza fasihi katika Andhra Pradesh.

Virejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. Prajasakti Newspaper from Hyderabad, India | ThePaperboy.com ..
  2. Prajasakti.com - Pra Jasa Kt I - PRAJASAKTI TELUGU NEWS PAPER .
  3. prajasakti.com - Site Info from Alexa Ilihifadhiwa 21 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine.
  4. Progesterone (www prajasakti com) Reviews Ilihifadhiwa 6 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]