Portland Tribune

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Portland Tribune
Port trib.JPG
Jina la gazeti Portland Tribune
Lilianzishwa 2001
Nchi Marekani Marekani
Mhariri Mark Garber
Mmiliki Kundi la Pamplin Media
Mchapishaji Steve Clark
Makao Makuu ya kampuni 6605 S.E. Lake Road
Portland, Oregon 97222-2161
Nakala zinazosambazwa 120,000
Tovuti Tovuti Rasmi ya Portland Tribune

Portland Tribune ni gazeti la kuchapishwa kila wiki linalochapishwa kila Alhamisi katika eneo la Portland,Oregon,Marekani.

Portland Tribune ni kipande cha Kundi la Pamplin Media, linalochapisha magazeti kadhaa ya kijamii katika eneo la Portland na ,pia, humiliki na huendesha stesheni ya redio ya majadiliano ya KPAM pamoja na stesheni zingine za redio katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Pacific.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mfaniyibiashara wa Portland, Robert B. Pamplin Jr. alitangaza nia yake ya kuanzisha gazeti hilo katika mwaka wa 2000. Toleo la kwanza la gazeti hili lililoanza kwa kuchapishwa mara mbili kwa wiki (Jumanne na Ijumaa) lilichapishwa 9 Februari 2001.Likiingia katika soko lililokuwa na magazeti kama The Oregonian (gazeti pekee la habari za jumla) na magazeti ya kila wiki: Willamette Week na The Portland Mercury. Wakati huo, ulikuwa mfano nadra sana wa upanuzi katika biashara ya magazeti kwa sababu kampuni nyingi za magazeti zilikuwa zikifungwa ama zikiungana. Uzinduzi wake ulitangulia kuteremka kwa matangazo katika magazeti. Hili likawa tatizo katika kuanzisha uchapishaji wa gazeti hili. Miezi kumi na moja baada ya uzinduzi,Portland Tribune lilipunguza shughuli zake za kuwasilisha magazeti hadi nyumbani za watu. Gazeti hili liliripotiwa kuleta hasara zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Ulipofika mwisho wa mwaka wa 2006, wafanyikazi wa chumba cha habari cha gazeti hili walipunguzwa hadi wakawa 27.

Mnamo 5 Mei 2008, jarida hili lilitangaza kuwa litaanzisha kuchapishwa mara moja kwa wiki, matoleo ya Alhamisi, huku likiambatana na kuandika habari kila siku katika tovuti yake rasmi.

Mnamo Julai 2009, "shida za kiuchumi" zilisababisha kufutwa kazi kwa waandishi wawili wa habari na kujiuzulu kwa mhariri msimamizi, na wafanyikazi wa chumba cha habari cha gazeti hili walipunguzwa wakawa 14.

Vipengele[hariri | hariri chanzo]

Jarida hili hujihusisha sana na masuala ya Portland na jimbo la Orego. Jarida hili linajulikana kwa kuandika habari za shule za upili za eneo hilo, timu za michezo hasa za NBA, Pac-10, Mkutano wa mchezo wa Big Sky na Mkutano wa mchezo wa Pwani Magharibi.

Portland Tribune huwa mdhamini wa Shindano la Portland Regional Spelling Bee la wanafunzi wa shule ya daraja la katikati. Mshindi wa shindano hili hushiriki katika Shindano la Scripps National Spelling Bee jijini Washington, D.C.

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]