Pori la Akiba la Klaserie
Mandhari
Pori la Akiba la Klaserie liko karibu na Mbuga ya Kruger na Mbuga ya Wanyama ya Timbavati, katika jimbo la Limpopo nchini Afrika Kusini . Lina eneo la takribani hektari 60,000 na Mto Klaserie unapita kwenye hifadhi hiyo.
Wanyamapori
[hariri | hariri chanzo]Aina za wanyamapori wanaopatikana ni pamoja na simba, tembo, faru mweupe, chui, duma, mbwa mwitu wa Kiafrika, fisi mwenye madoadoa, nyati na swala.