Ponta Jalunga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ponta Jalunga

Ponta Jalunga ni rasi iliyopo Kaskazini Mashariki mwa bandari ya Furna, kisiwa cha Brava kusini magharibi mwa Cabo Verde. Ni sehemu ya kaskazini mashariki kabisa ya kisiwa hicho. Ni eneo lenye miamba, hadi mita 120 kwa urefu. Ilitajwa kama "Pt. Ghelongo" katika ramani ya 1747 iliyochorwa na Jacques-Nicolas Bellin. [1]

Mnara wa Taa Ponta Jalunga[hariri | hariri chanzo]

Mnara wa taa unaopatikana Ponta Jalunga ulijengwa mnamo mwaka 1891. Ni mnara mweupe kwa uashi. Una urefu wa mita 8 na uko mita 26 juu ya usawa wa bahari. Masafa yake yanaenea hadi nautical mile 5 (km 9.3; mi 5.8) na chanzo cha nuru yake, kama ilivyo kwa taa nyingine nyingi, zinaendeshwa kwa jua.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ponta Jalunga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.