Pogromu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Pogromu (kutoka rus. погромить (pogromit) - kuharibu vikali, kufanya fujo) ni neno la kutaja ghasia kali inayolengwa dhidi ya kundi maalumu kama vile wafuasi wa dini au kabila fulani.

Neno latokana na ghasia za fujo katika Urusi wa karne ya 19 ambako Wayahudi walishambuliwa, maduka na nyumba zao kuharibiwa na idadi ya watu kuuawa hovyo. Kwa hiyo neno "pogromu" lataja hasa mashambulio dhidi ya Wayahudi katika Ulaya. Lakini inatumiwa pia kwa mashambulio dhidi ya vikundi vingine.