Peter Abrahams

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Peter Abrahams iliyochukuliwa na Carl Van Vechten, 1955

Peter Abrahams (amezaliwa 3 Machi 1919) alikuwa mwandishi wa vitabu vya riwaya kutoka Afrika Kusini. Alihama Afrika Kusini mwaka wa 1939, na tangu 1956 aliishi nchini Jamaika. Riwaya zake zahusu hasa vipengele mbalimbali vya ubaguzi wa rangi.

Maisha ya awali na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Abrahams alizaliwa mnamo 1919 huko Vrededorp, kitongoji cha Johannesburg, Afrika Kusini; baba yake ni mtu wa Ethiopia na mama yake alikuwa Mkoloni, mwenye mizizi ya Kifaransa na Kiafrika.[1] Abrahams alikuwa na umri wa miaka mitano wakati baba yake alipofariki, na baada ya hapo familia yake ilihangaika kifedha mama yake alimpeleka kwenda kuishi na ndugu zake hadi umri wa miaka 11, alipokuwa mwanafunzi wa bweni katika Shule ya Kanisa la Anglikana la Grace Dieu huko Pietersburg. [2] Baada ya kuhitimu kutoka hapo, alienda Shule ya Sekondari ya St Peter huko Rosettenville, akilipia ada yake ya masomo kwa kufanya kazi katika Kituo cha Jamii cha Wanaume wa Bantu.[1]

Riwaya zake[hariri | hariri chanzo]

  • Mine boy (1946)
  • The path of thunder (1948)
  • Wild conquest (1950)
  • Tell freedom (1954; tawasifu)
  • A wreath for Udomo (1956)
  • A night of their own (1965)
  • This island now (1966)

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • (en) Chapman, Michael. 2003. Southern African Literatures, University of Natal Press. ISBN 1-86914-028-1
  • (de) Seiler-Dietrich, Almut. 1984. Die Literaturen Schwarzafrikas [Fasihi za Kiafrika]. ISBN 3-406-09499-6
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Peter Abrahams kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. 1.0 1.1 J. Brooks Spector, "Politically incorrect since 2009" Archived 7 Machi 2021 at the Wayback Machine., PAWA website.
  2. Gikandi, Simon (2003). Encyclopedia of African Literature. Taylor & Francis. uk. 5. ISBN 978-1-134-58223-5. Iliwekwa mnamo 12 October 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)