Pera

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kwa maana mengine ya jina hili angalia Pera (maana)
Pera

Pera ni tunda la mpera.

Kulingana na aina ya mpera, tunda lina urefu wa sentimita 4 hadi 12. Ladha inaweza kufanana kiasi na ganda la limau lakini si kali vile.

Ngozi ya tunda inaweza kuwa nene au nyembamba, wakati mwingine huwa na ladha chungu. Rangi ya tunda ni kibichi kabla ya kuiva, tangu kuiva huwa njanonjano. Nyama yake hutokea kwa ladha baina ya chachu na tamu, rangi yake baina nyeupe hadi nyekundu.

Katikati kuna mbegu nyingi ambazo ni ndogo na ngumu.